Tuesday, May 2, 2017

WAHAMIAJI HARAMU 411 WAKAMATWA BAGAMOYO ,KIPINDI CHA MIEZI SITA ILIYOPITA

D
Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza jambo baada ya kupatiwa taarifa ya kuingia kwa wahamiaji haramu 72, huko Bagamoyo
D 1
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, alhaj Majid Mwanga akitolea ufafanuzi tatizo la wahamiaji haramu wilayani hapo. (picha na Mwamvua Mwinyi) 
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo 
Jeshi la polisi limewakamata wahamiaji haramu 72 raia kutoka nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali. 
Aidha katika kipindi cha miezi sita,wahamiaji haramu 411 kutoka maeneo mbalimbali,walikamatwa wilayani Bagamoyo.  
Kamanda wa polisi wilaya ya Bagamoyo Adam Maro, alimwambia mkuu wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, kwamba wahamiaji hao walikamatwa usiku wa kuamkia jana .
Alieleza wahamiaji hao walikutwa wakiwa wametelekezwa na mwenyeji wao aliyekuwa akiwasafirisha kutoka Ethiopia kwenda Afrika Kusini kwenye eneo la pembezoni kidogo mwa fukwe ya bahari ya hindi katika kata ya Nianjema. 
Kamanda Maro, alisema matukio ya wahamiaji wanaoingia bila kibali na magendo kupitia Bagamoyo yamekuwa yakitokea mara kwa mara kutokana na njia za panya hasa bahari . 
Nae mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, alhaj Majid Mwanga, alisema tatizo la kuingia kwa wahamiaji haramu katika mwambao wa bahari ya Hindi na kupitia bandari bubu zilizo wilaya hiyo. 
Akizungumza baada ya kupatiwa taarifa hiyo, mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Ndikilo, alitoa onyo kwa watu wanaofanya biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu . 
Mhandisi Ndikilo, alibainisha wasafirishaji hao waache tabia hiyo mara moja kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.

No comments :

Post a Comment