Tuesday, May 2, 2017

Wafanyakazi TBL Group washiriki maandamano ya Mei Mosi na ujumbe mzito kuelekea uchumi wa viwanda


Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group wameungana na wafanyakazi wa taasisi nyingine kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo kwa hapa nchini ilifanyika mkoani Kilimanjaro ambapo mgeni wa heshima alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.John Magufuli.
Katika kuadhimisha siku hiyo muhimu kwao wafanyakazi walishiriki katika maandamano yaliyofanyika sehemu mbalimbali za nchi na kauli mbiu yao ya mwaka huu “Uchumi wa Viwanda uzingatie haki,Maslahi na heshima ya wafanyakazi.
Kampuni ya TBL Group ina viwanda katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Arusha,Kilimanjaro na Mbeya
im1
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakiwa katika maandamano ya Mei Mosi Mjini Moshi kuelekea uwanja wa Ushirika
im2
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakiwa katika maandamano ya Mei Mosi Mjini Moshi kuelekea uwanja wa Ushirika
im4 im5
Vitendea kazi kama magari pia yalionyeshwa katika maandamano ya Mei Mosi
im6
Wafanyakazi wa TBL Group ndani ya uwanja wakipita jukwaa kuu
im7
Wafanyakazi wa TBL Group ndani ya uwanja wakipita jukwaa kuu

No comments :

Post a Comment