MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewaachia huru wabunge wa
Ukawa na makada wa muungano huo baada ya kuona kuwa hawana kesi ya kujibu.
February
27 2016 katika ukumbi wa Karimjee Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea,
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara,
Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema, mfanyabiashara na kada wa chama hicho,
Rafii Juma na Diwani wa Kata ya Saranga Kimara, Ephreim Kinyafu walidaiwa
kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa
upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha, hata mlalamikaji Mmbando hakumbuki ni
nani aliyemjeruhi.
Aidha ameongeza
ushahidi wake ulielezea Jinsi washtakiwa walivyojishughulisha na nyaraka siku
ya tukio na siyo kumjeruhi, hivyo hakimu aliwaachia huru washtakiwa wote kwa
kuwa hawana kesi ya kujibu.
No comments :
Post a Comment