Wajumbe wa Kikao cha Pamoja kati
ya Chama cha Ushirika cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane kilichopo
eneo la Maruhubi mjini Unguja na ugeni wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB). Kikao kilijadilia changamoto zinazozikabili Ushirika
huo na namna TADB inavyoweza kuwasaidia katika kuendeleza ushirika huo.
Mtaalamu wa Ushirika kutoka Wizara
ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Bw. Khamis Mkanga
(katikati) akiendesha Kikao cha Pamoja kati ya Chama cha Ushirika cha
Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane kilichopo eneo la Maruhubi mjini Unguja
na ugeni wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akizungumza na Wanaushirika wa Chama
cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane wakati alipofanya kikao na umoja
huo. Kikao hicho kilifanyika eneo la Maruhubi mjini Unguja. Wengine
pichani ni Mwenyekiti wa Ushirika huo Bw. Haji Omar Haji na Mtaalamu wa
Ushirika kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar,
Bw. Khamis Mkanga (wapili kushoto).
Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo
wa TADB, Bw. Augustino Chacha (wakwanza kushoto) akizungumza na
Wanaushirika wa Chama cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane kuhusiana na
mikopo na huduma zinazotolewa na TADB.
Mmoja wa Wanaushirika wa Chama cha
Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane, Bibi Bahati Shabani (kulia) akitoa
maelezo kuhusu shughuli za uchakataji wa dagaa. Bibi Bahati alimuelezea
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto)
changamoto wanazokabiliana nazo katika shughuli hiyo.
Bw. Salim Kassim (wapili kulia)
Mmoja wa Wanaushirika wa Chama cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane
akifafanua jambo kwa ugeni kutoka TADB.
Ugeni kutoka TADB wakkaua dagaa walio tayari kuuzwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Francis Assenga (kushoto) akmuunga mkono kwa kununua dagaa zungumza
mmoja wa Wanaushirika wa Chama cha Wauza Madagaa cha Tusiyumbishane.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Francis Assenga (kulia) akishauri namna bora ya ufungishaji wa
dagaa walio tayari kwenda sokoni.
……………………………………
Na mwandishi wetu, Zanzibar
Chama cha Ushirika cha Wauza
Madagaa cha Tusiyumbishane kilichopo eneo la Maruhubi mjini Unguja
kimeiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika
kuendeleza ushirika wao kwa kuwapatia mikopo na mahitaji mengine ili
kuboresha huduma zao.
Akizungumza katika kikao cha
pamoja kilichofanyika katika eneo la ushirika huo mjini Unguja,
Mwenyekiti wa Tusiyumbishane, Bw. Haji Omar Haji amesema licha ya fursa
kubwa iliyopo kwenye eneo la ukaushaji wa madagaa, ushirika wao
unakabiliwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji
wa fedha za mtaji kwa ajili ya kuboresha huduma zao.
Bw. Haji ameongeza ukosefu wa
mikopo ya uhakika imekuwa ni changamoto kubwa inayochangia kurudisha
nyuma ukuaji wa biashara hiyo hivyo kuwa kikwazo katika kupambana na
umaskini wa kipato miongoni mwa washirika wa umoja huo hivyo akaiomba
benki hiyo kuwawezesha ili kuongeza tija ya shughuli zao.
“Uduni wa mitaji ya uhakika
inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabenki na taasisis nyingine za kifedha
kushindwa kutuwezesha sie wajasiriamali wa hali ya chini kwa kukosa
sifa wazitakazo, hivyo tunaiomba TADB kutuwezesha ili tuongeze tija
katika shughuli zetu,” Bw. Haji aliongeza.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki yake imesikia
kilio cha umoja huo, na watatimiza ndoto zao ili kuweza kutimiza ndoto
za Serikali za kuanzisha TADB ili kusaidia wakulima na wavuvi wadogo
kukabiliana na mapungufu ya upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo
na uvuvi kuchagiza mapinduzi katika kilimo nchini.
Bw. Assenga ameongeza kuwa sekta
ya uvuvi hasa ufugaji wa samaki ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo
inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo
mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa mazao yatokanayo na
samaki nchini.
Ameongeza kuwa Benki yake
imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa eneo la uvuvi na ufugaji
wa samaki ili kuongeza tija kwa wakulima na wafugaji wa samaki wadogo
nchini.
“Benki inatoa mikopo na kusaidia
uwekezaji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya masoko kwa ajiili ya
kuboresha kilimo na uvuvi hasa ufugaji wa samaki nchini,” alisema Bw.
Assenga.
No comments :
Post a Comment