Mwanasheria na Msimamizi wa Mradi wa
Uwezeshaji Shirikishi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani nchini
Tanzania, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina kwa Viongozi
wa serikali za mitaa kutoka wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani
Mwanza.
Semina hiyo ya siku tatu, kuanzia jana
Mei 09 imewashirikisha Madiwani, Watendaji wa Kata, Maafisa Maendeleo na
Ustawi wa Jamii, Wenyeviti wa Mitaa na dawati la jinsia kutoka jeshi la
polisi imelenga kuwajengea uwezo viongozi hao ili kusaidia kutetea na
kulinda maslahi ya mtoto mfanyakazi wa nyumbani na kumuepusha na
utumikishwaji wa kazi ngumu na maslahi duni.
#BMGHabari
Mwanasheria wa Shirika la WOTESAWA,
Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina hiyo ambapo pia
ameelezea juu ya umuhimu wa viongozi hao kuitambua Sheria ya Ajira na
Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 ambayo inakataza mtoto chini ya umri wa
miaka 14 kuajiriwa huku wale walio juu ya umri huo wakipaswa kuajiriwa
kufanya kazi zisizo hatarishi.
Aidha amekumbusha juu ya kuutambua Waraka wa Mishahara wa mwaka 2013 ambao unaelekeza
kwamba mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa kiwango cha
chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri ni balozi
ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi kwenye
nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye
nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni rai
wakigeni.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akichangia mada
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
Semina hiyo ilianza jana Mei 09,2017 na inatamatika kesho Mei 11,2017 Jijini Mwanza
Waraka wa Mishahara wa mwaka 2013 kwa wafanyakazi wa nyumbani
Afisa kutoka shirika la WOTESAWA akiwa kwenye semina hiyo
Diwani wa Kata ya Buhongwa Jijini
Mwanza, John Kabadi, amesema semina hiyo itwasaidia katika kutetea
maslahi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani ikiwemo kuwaepusha na
utumikishwaji pamoja na ujira duni.
Gloria Shindika kutoka dawati la jinsia,
kituo cha polisi Igogo Jijini Mwanza, amesema semina imewaongezea mbinu
zaidi za namna ya kuwasaidia watoto wafanyakazi wa nyumbani watakaokuwa
wakikumbwa na aina yoyote ya utumikishwaji.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamanoro
Kaskazini, Kata ya Ibungilo Manispaa ya Ilemela, ameeleza kutumia elimu
aliyoipata kwenye semina hiyo katika kuwaelimisha wananchi wa mtaa wake
katika kuhakikisha maslahi na haki za mtoto yanalindwa
Mwanasheria wa Shirika la WOTESAWA, Jackline Ngallo, akizungumza na Lake Fm Mwanza
Shirika la WOTESAWA linawahimiza
wanajamii kwamba bado watoto wafanyakazi wa nyumbani wanayo haki ya
kupata elimu hivyo ni vyema haki hiyo ikazingatiwa.
No comments :
Post a Comment