Tuesday, May 9, 2017

KILIO TENA ARUSHA:WATANO WAFA KWA KUANGUKIWA NA MTI

 NA VERO IGNATUS, ARUSHA
WATOTO watano wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuangukiwa na mti wilayani Arumeru mkoani Arusha leo Mei 9, 2017.
Taarifa za kipolisi zinasema, watoto hao wa familia mzee Jonathani Kalambiya,(55) mkazi wa sokoni II katika kijiji cha kinyeresi wilayani Arumeru Mkoani Arusha imekutwa na umauti huo baada ya mti
mkubwa uliong’olewa na maji ya mafuriko ya mvua kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote watano.
Mkasa huo wa kusikitisha ulitokea usiku wa kuamkia leo Mei 9, 201.
Kamanda wa polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja watoto waliokufa katika tukio hilo ni pamoja na watoto wawili wanafunzi wa mzee huyo ambaye ni mlinzi wa hospital ya ya Dkt. Mohamed ya Jijini Arusha.
Mkumbo aliwataka wanafunzi ambao ni watoto wa mzee Kalambwia ambaye siku ya tukio alikuwa kazini ni pamoja na Miliamu Jonathani(16) mwanafunzi wa kidatu cha pili wa shule ya sekondari ya Inaboishu, Grolia Jonathani(11) mwanafunzi wa shule ya msingi Kinyeresi iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha,
Image result for charles mkumboGiliad  Jonathani(31), Lazaro Lomnyaki
(26) na Best Jonathani(20).
Kamanda Mkumbo alisema kuwa mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake mana uliangukia nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Jiji la Arusha na Mkoa kwa ujumla.
Tukio hilo linakuja siku chache baada ya ajali ya kusikitisha iliyoua wanafunzi wa shule ya msingi Lucky Vincent wapatao 33, walim,u wawili na dereva wa gari la shule baada ya basi walilokuwa wakisafiria kwenda wilayani Karatu kupata ajali eneo la Rothia wilayani humo.
 Mti ulioanguka ukang’ookana shina lake na kuangukia nyumba na kusababisha
maafa hayo ya watu watano wa familia moja.
Jitihada za uokozi zikiendelea 
Miili ikiwa imeshapakiwa ndani ya gari la polisi

No comments :

Post a Comment