Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa
Kampuni ya Coca Cola Kwanza, Nalaka Hettiarachchi (katikati) akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mashindano ya Dasani
Marathon yanayotarajia kufanyika Mei 14 mwaka huu Jijini Dar es
Salaam,Kushoto kwake ni Rais
wa Chama Cha Wakimbiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Goodluck Elvis na kulia kwake ni
Mwanariadha wa zamani wa Kimataifa, Juma Ikangaa.wa Chama Cha Wakimbiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Goodluck Elvis na kulia kwake ni
…………………..
Husna Saidi na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
MWANARIADHA wa zamani wa
Kimataifa, Juma Ikangaa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya
riadha ya Dasani Marathon yanayotarajia kufanyika Jijini Dar es Salaam
tarehe 14 Mei mwaka huu.
Mashindano hayo ya umbali wa kilometa 10 na 21 yanatarajia kushirikisha zaidi ya wanariadha 1000 kutoka Mikoa mbalimbali nchini.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar
es Salaam na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Coca Cola
Kwanza, Nalaka Hettiarachchi alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu mashindano hayo yaliyolenga kukuza mchezo wa riadha na
kujenga afya kwa wanamichezo.
Hettiarachchi alisema kuwa
wameamua kudhamini shindano hilo kama njia moja wapo ya kushiriki katika
shughuli za kijamii pia kwa sababu lina lengo la kukuza vipaji vya
wanariadha wa Tanzania ili kuwawezesha kutamba katika mashindano ya
Kimataifa.
“Mashindano haya yatadhaminiwa na
kampuni ya Coca Cola kwanza kupitia kinywaji chetu cha maji ya dasani,
ambapo wakati wa kukimbia wanariadha watakuwa na wakati wa kupata maji
ya kupoza koo” alisema Hettiarachchi.
Kwa upande wake Rais wa Chama Cha
Wakimbiaji Mkoa wa Dar es Salaam , Goodluck Elvis alisema mashindano
hayo yatashirikisha wakimbiaji wa wanaume na wanawake wa rika tofauti na
washindi watajipatia zawadi za fedha taslimu pamoja na medali kwa
watakaomaliza mbio.
“Mbio hizo za kilomita 10 na
kilomita 21 zitakazoanzia na kuishia katika bwalo la Maofisa wa Polisi –
Masaki usajili wake unaendelea kufanyika katika maeneo ya Colosseum
Gym, Masaki, Shoppers Supermarket, Mikocheni na Mlimani City Mall,”
alisema Elvis.
Aidha, alifafanua kuwa gharama za
usajili kwa ajili mashindano hayo ni Tsh. 30,000 kwa kila mshiriki
ambapo mshiriki atapatiwa begi na fulana kwa ajili ya kushiriki katika
mashindano hayo.
Mashindano hayo yameanzishwa miaka
mitatu iliyopita na yameendelea kufanya vizuri mwaka hadi mwaka,
Kampuni ya Cocacola inategemea kutoa ufadhili katika mashindano hayo kwa
zaidi ya miaka mitano ijayo.
No comments :
Post a Comment