Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua jengo la kituo cha
Polisi kata ya Iselamagazi ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi
wakishirikiana na mbunge wao wa Solwa Ahmed Salimu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa maelekezo kwa
watendaji wa kata,vijiji,vitongoji,viongozi wa Sungusungu na Madiwani
wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga juu ya kutumia jengo hilo
kikamilifu kutoa taarifa ya waharifu na kuchukuliwa hatua kali za
kisheria
Ukaguzi wa jengo ukiendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishukuru wananchi kuhusu
ujenzi wa jengo hilo ambalo limejengwa kwa haraka ambapo ujenzi ulianza
Januari 12,2017 na limegharimu shilingi milioni 13.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro baada ya kumaliza kukagua
jengo hilo la kituo cha polisi. Matiro aliwaahidi kuwaezekea paa ili
lianze kufanya kazi haraka na kumaliza matukio ya uharifu kwenye tarafa
hiyo ya Nindo na kudumisha amani kwa wananchi wote wakiwemo watumishi wa
serikali.
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akiteta jambo na viongozi wa serikali
pamoja na baadhi ya madiwani wa halmashauri kabla ya kuingia kwenye
mkutano wa viongozi wa Sungusungu na watendaji wa vijiji,kata na
vitongoji kujadili ajenda mbili za ulinzi na usalama pamoja na kuunda
ushirika wa vyama vya kuuza mazao ili kuinua wakulima kiuchumi sambamba
na kuhifadhi chakula cha akiba ili kukabiliana na janga la njaa hapo
baadae.
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akizungumza na viongozi wa
Sungusungu,baadhi ya watendaji wa kata ,vijiji,vitongoji na Madiwani wa
halmashauri hiyo juu ya kudhibiti uhalifu kwenye tarafa hiyo ya Nindo
pamoja na kuwafichua wahalifu ambao huhatarisha hali ya amani.
Wajumbe wakisikiliza maagizo ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro kuhusu namna ya kudumisha amani na kutunza chakula cha akiba na
kutokubali kulanguliwa mazao yao mashambani na wafanyabiashara na
kuwafanya kuendelea kuwa maskini.
Ofisa Tarafa ya Nindo Budugu Kasuka akitoa taarifa ya masikitiko kwa
mkuu wa wilaya juu ya baadhi ya wananchi ambapo wamekuwa wakivamia
watumishi wa serikali hasa walimu kwa kupora mali zao na kisha kuwa kata
kata mapanga hali ambayo iliyowagusa wananchi wengi na kuamua
kuchangisha pesa ili kujenga kituo cha polisi ambacho kitasaidia
kudhibiti waharifu kwenye tarafa hiyo na kubainisha kuwa kituo hicho
kitakuwa kimekamilika mwezi Juni 30 mwaka huu.
Kikao kikiendelea huku wajumbe hao wakilitupia lawana jeshi la polisi
kuwa pale wanapopelekewa waharifu hususani wale wanaotuhumiwa kukata
mapanga walimu ambapo wao wamekuwa wakiwapatia dhamana na kisha kurudi
mitaani kuanza kuwatambia na pia kuendeleza uharifu kama kawaida na
hivyo kukata tamaa na kuogopa kutoa tena taarifa polisi licha ya kuwajua
watu wote wanaofanya vitendo hivyo.
Hapa wajumbe wakisikiliza majibu kutoka kwa kaimu kamanda wa jeshi la
polisi wilaya Shadrack Zambi ambaye hayupo pichani kwa kufafaunua kuwa
kila mtu ana haki ya kupewa dhamana, huku akibainisha watuhumiwa wote
waliowakamata na kuwapeleka kwao kesi zao zinaendelea kusikilizwa
mahakamani na endapo wakibainika kukutwa na makosa hayo watachukuliwa
hatua za kisheria na pia kuwasisitiza wasichoke kutoa taarifa za
waharifu ,huku akiwapongeza kwa ujenzi wa kituo hicho cha polisi ambacho
kitasaidia kuongeza idadi ya askari wengi na hatimaye kufanikiwa
kukomesha uharifu kwenye tarafa hiyo ya Nindo
(Picha zote na Marco Maduhu Malunde1 blog)
No comments :
Post a Comment