Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa
Baraza la Habari Tanzania {MCT} uliofika Ofisini kwake Vuga Mjini
Zanzibar kubadilishana nao mawazo. Kulia ya Balozi Seif ni Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga na Kushoto ya Balozi
ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania { MCT } upande wa
Zanzibar Bibi Shifaa Hassan .
Mkuu wa
Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania { MCT } upande wa Zanzibar Bibi
Shifaa Hassan akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif walipokutana nae kwa mazungumzo.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga Kulia ya Balozi Seif
akielezea mikakati ya Baraza la Habari Tanzania inavyofanya kazi
Zanzibar katika kuhakikisha Maadili ya Habari yanazingatiwa na Wana
Habari wote Nchini.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga akimkabidhi Balozi
Seif Vitabu mbali mbali vilivyochapishwa na Baraza hilo kuhusu Tasnia
ya Habari Tanzania.
Balozi
Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa juu wa Baraza la Habari
Tanzania mara baada ya kubadilishana mawazo Ofisini kwake Vuga Mjini
Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari
Bwana Kajubi Mukajanga na Muandishi wa Makala wa MCT Yussuf Mpinga.
Kulia
ya Balozi Seif ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania { MCT }
upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan, Muhariri wa Machapisho wa MCT
Khamis Mzee na Mkuu wa Kitengo cha Rasilmali Watu cha MCT Bivi Ziada
Kilobo. Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
inasubiri kuyapokea kwa ajili ya kuyafanyia kazi mapendekezo
yatakayowasilishwa ya Rasimu ya Sera ya Habari Zanzibar katika kuona
Sekta ya Habari Nchini inakuwa imara.
Alisema Taasisi
zinazohusika na jukumu la kusimamia masuala hayo ni vyema zikahakikisha
kwamba zinaharakisha mapendekezo hayo ili ile dhana ya Uhuru wa kupata
Habari bila ya kuogopa inapatikana.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa
kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Uongozi wa Baraza la Habari
Tanzania { MCT } ulioongozwa na Katibu Mtendaji wake Bwana Kajubi
Mukajanga aliokutana nao hapo Afisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
Alisema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutoa kila aina ya msaada
katika kuona Sekta hiyo muhimu kwa jamii inawajibika ipasavyo katika
kuwapasha Habari Wananchi.
Pages
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment