NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MFUKO
wa Pensheni wa PPF unashiriki katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi
kiuchumi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Mafao yanayotewa na Mfuko huo
Maonnesho
hayo yalifunguliwa rasmi Aprili 18, 2017 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
Kwa
mujibu wa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Bi. Janeth Ezekiel, Mfuko huo unatoa
Mafao mbalimbali na katika Maonesho haya utajikita zaidi katika kutoaa elimu
juu ya mfumo wa ' Wote scheme' unaowezesha watu kutoka sekta isiyo rasmi kuwa
wanachama.
“Wote
Scheme unawahusu wale wote wanaojiajiri kama vile mama lishe, madereva wa boda
boda, wakulima, wafugaji, wajasiriamali, wasanii, wote hawa wanaweza
kujiunga na mpango huo ambapo pamoja na mambo mengine watafaidika kwa kuwa na fursa
za huduma za afya, mikopo ya maendeleo, mikopo ya Elimu na Mafao ya uzeeni.”
Alisema Bi. Janeth
Kupitia
Maonesho haya PPF inasajili wanachama wapya hapo hapo viwanjani
pamoja na kukabidhi vitambulisho vya uanachama wa “Wote Scheme”
Hivyo
ni fursa muhimu kwa wakazi wa Dodoma kufika katika viwanja vya Mashujaa kupata
elimu hii muhimu na kujiunga na Mfuko huu, alsiema. Aidha alisema kwa
wale ambao hawapo Dodoma, wanaweza
kutembelea Ofisi za PPF zilizopo karibu nao.Katika maonesho hayo
yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,
(NEEC), Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, alimkabidhi cheti cha
udhamini, Meneja wa PPF Kanda ya
Mashariki na Kati, Bw.Michael Christian ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa
PPF, Bw. William Erio.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Bi.
Janeth Ezekiel, (kushoto), akitoa maelezo ya shughuli mbali mbali
zitolewazo na PPF kwa wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo wakati
wa Maonesho hayo yanayoedelea kwenye viwanja vya Mashujaa mkoani Dodoma
leo Aprili 19, 2017
Afisa
Mfawidhi wa PPF Astro Liganga akimfafanulia Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matilo fursa apatazo mwanachama aliyejiunga na PPF kupitia Mfumo wa “Wote
Scheme”
Wananchi wa kada mbalimbali wakitembelea banda la PPF kwenye maonesho hayo
Meneja
wa PPF, Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian, (kushoto), akimuelezea kazi
za PPF mmoja wa watu waliotembelea Maonesho hayo
Maafisa wa PPF wakiwasikiliza kwa makini wananchi waliotembelea banda hilo
Picha ya pamoja







No comments :
Post a Comment