Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa
pili kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na
wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao cha
Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa
pili kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na
wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao cha
Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bw. Shukuru
Sikunjema, akitoa maoni yake kwa Mwenyekiti Wa Baraza la Wafanyakazi
Eng. Joseph Nyamhanga katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani
Morogoro.
Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) wakifuatilia maelekezo ya
Baraza la Wafanyakazi wakati wa kikao hicho kilichofanyika Mkoani
Morogoro.
Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Wakiimba nyimbo ya
‘Solidarity forever’ kuonyesha mshikamano katika utendaji kazi wakati wa
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya kufunga kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika
Mkoani Morogoro.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
…………..
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.Joseph Nyamhanga,
amewataka watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza majukumu yao kwa weledi
na
uadilifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya Awamu ya
Tano.
Akisoma hotuba ya ufunguzi kwa
niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Profesa Makame Mbarawa, katika kikao cha
Baraza la Wafanyakazi leo, mkoani Morogoro, Eng. Nyamhanga, ametoa wito
kwa watumishi wote kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza majukumu
yao ili kuleta tija kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.
“Naliomba baraza hili la
wafanyakazi kuhakikisha linahamasisha watumishi wote wa Wizara
kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, weledi na ushirikiano
ili kuleta ufanisi”, amesema Eng.Nyamhanga.
Aidha, Eng. Nyamhanga
amelisisitiza Baraza hilo kuandaa mkataba wa kupima utendaji kazi wa
watumishi katika majukumu yao ya kila siku ili kupima ufanisi wa
watumishi hao kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini.
Katibu Mkuu Nyamhanga , amelitaka
Baraza hilo kuweka mazingira maalum kwa watumishi ikiwemo kuandaa
mpango wa mafunzo ya ndani na nje ya nchi ili kuongeza ujuzi kwa
watumishi wa Wizara hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Chama cha Wafanyakazi Tawi la Ujenzi Bw. Samuel Mticco, amemhakikishia
Katibu Mkuu huyo kutekeleza maagizo yote yaliyosemwa katika Baraza hilo
ikiwemo la uandaaji wa mkataba wa utendaji kazi kwa watumishi.
Kikao hicho cha siku moja cha
Baraza la wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi pamoja na mambo mengine
kimekubaliana kupunguza matumizi ya fedha za Serikali yasiyo ya lazima
pamoja na kupambana na vitendo vya ufisadi na rushwa.
Imetolewa na kitengo cha mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments :
Post a Comment