Judith Ferdinand, BMGHabari
Wakazi
wa Jiji la Mwanza na viunga vyake, wanatarajia kupata burudani ya
kukata na mundu kutoka kwa wasanii mbalimbali Kanda ya Ziwa katika
tamasha la burudani “Nyanza Festival 2017”.
Burudani
hiyo ambayo itakua ya aina yake kwa kuwakutanisha wasanii kutoka mikoa
ya Kanda ya Ziwa, itafanyika Siku Kuu ya Pasaka kuanzia saa nne asubuhi
mpaka majogoo kwa kiingilio cha shilingi 5,000 tu katika Uwanja wa CCM
Kirumba.
Mratibu
wa tamasha hilo, Fabian Fanuel, amesema mbali na burudani ya mziki pia
kutakua na mchezo wa mpira wa miguu kati ya Waandish wa habari za
michezo Kanda ya Ziwa LASPOJA Fc na Bongo Movie, na Madjs na Watangazaji
wa vipindi vya burudani watacheza na wafanyakazi wa halmashauri ya Jiji
la Mwanza.
Naye
Afisa Habari wa tamasha hilo, George Binagi, amebainisha kwamba
wanatasnia wa burudani hususani wanamuziki mastaa na chipukizi kutoka
mikoa ya Kanda ya Ziwa, wameahidi kudondosha burudani kali siku hiyo.
“Zaidi
ya wasanii 30 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa tayari wamethibitisha
kupanda jukwaa la Nyanza Festival 2017 hivyo niwasihi wapenzi wa
burudani wakae tayari kwa burudani hiyo ambapo kiingilio itakuwa elfu
tano tu”. Amesema Binagi.
Nyanza
Festival ni tamasha lililoasisiwa na Wanatasnia mbalimbali kutoka Kanda
ya Ziwa wakiwemo wanamuziki, watangazaji, waandishi wa habari, Madjz na
wadau wengine wengi kupitia umoja wao wa Mwanza.Com chini ya kampuni ya
Famara Entertainment, lengo likiwa ni kuukuza na kuuendeleza zaidi
muziki wa Kanda ya Ziwa.
No comments :
Post a Comment