Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia
Happiness Seneda akionyeshwa eneo lililopo kata ya Mwendapole na
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Namelok Janet Mwasuka wa kushoto
ambapo kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa ajili ya wasicahna na
wanawake wajasiriamali waliopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia
Happiness Seneda kulia akiwa amemshika mmoja wa watoto huku akisikiliza
maelekezo kuhusina na ujezni wa kiutuo hicho maalumu cha elimu kwa ajili
ya wasichan na wakinamama kinachijengwa katika kata ya Mwendapole
Wilayani Kibaha, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Namelok Janet
Mwasuka
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya
Nameloc akoinyesha eneo ambalo kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa
ajili ya wasichana na wanawake wajasiriamali katika kata ya Mwendapole
Wilayani Kibaha Mkoani Pwani (PICHA NA VICTOR MASANGU)
………….
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
KATIKA kuunga juhudi za serikali
ya awamu ya tano kupambana na wimbi la umasikini taasisi ya Namelok ya
Wilayani Kibaha inatarajia kujenga kituo maalumu cha wasichana na
wanawake wajasiriamali ambacho kitakuwa kinajihusisha na masuala ya
utoaji wa mafunzo mbali mbali kwa lengo la kuweza kuwapa fursa ya
kuachana na kuwa tegemezi na kujiajiri wao wenyewe.
Akizungumza katika sherehe za
uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho zilizofanyika katika Kata ya
Mwendapole iliyopo katika halmashauri ya mji wa Kibaha Mkurugenzi
mtendaji wa taasisi hiyo Janet Mwasuka amesema kukamilika kwa ujenzi
huo kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa kuwainua wanawake hao
kiuchumuni kupitia mafunzo ya stadi za kazi pamoja na fursa zilizopo
kutokana na elimu watakayoipata.
Janet alibainisha kuwa anatambau
kuwa wanawake wegine katika Wilaya ya Kibaha ambao baadhi yao
wameshindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa elimu ya ujasiriamali
hivyo ana imani kituo hicho kitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuleta
mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wanawake pamoja na jamii yote kwa
ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa
ya kiserikali ya Purple Planet ya Jijini Dar es Salaam
inayojishughulisha na kuwasaidia katika kuendesha biashara zao na
kuwainua kiuchumi wanawake wajasiriamali Hilda Kisoka amebainisha kuwa
mikakati yao waliyojiwekea ni kufika mbali zaidi na kuuza bidhaa
wanazozizalisha hapa nchini hadi nje ya nchi kwa lengo la kujitangaza
zaidi.
Alisema kwamba ana imani wanawake
wengi hapa nchini wana uwezo mkubwa wa kuengeneza bidhaa zenye ubora wa
hali ya juu hivyo ameiomba serikali ya awamu ya tano kuwasaidi kwa hali
na mali ili kuweza kufika mbali katika kuleta ushindani zaidi wa masoko
katika nchi zingine za nje na kuondokana na kuwa tegemezi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Kisarawe Happiness Seneda ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi
huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani amekemea vitendo vya wanawake
kufayiwa vitendo vya ukataili na unyanyasaji na kujikuta baadhi yao
wanashindwa kutimiza ndoto zao na malengo yao waliyojiwekea katika siku
za baadae.
“Jamani mimi mwenyewe nimeshuhudia
baadhi ya maeneo kuna watu wanafanya vitendo vya ukatili na
kuwanyanyasa wanawake yani hili suala kwa upande mimi kwa kweli
silipendi kwa sababu baadhi ya wanawake wanashindwa kutimiza malengo yao
ambayo yamejiwekea kwa hiyi katika hili sisi kama serikali ni lazima
tulivalie njuga ii kuondokana na hali hii,”alisema Seneba
Pia katika hatua nyingine alitoa
wito kwa wakinababa wote katika Mkoa wa Pwani kuachana na vitendo hivyo
vya kuwanyanyasa wanawake na kuwapiga bila sababu zozote za msingi na
badala yake wabadilike na kuhakikisha kwamba wanawasaidia kuwawezesha
katika shughuli zao mbali mbali za ujasiriamali kwa lengo la kuweza
kupambana na wimbi la umasikini.
KITUO hicho ambacho kinajegwa
katika kata ya Mwendapole kinatarajiwa mpaka kukamilika kwake kugharimu
kiasi cha shilingi milioni 45 na katika awamu ya kwanza kinatarajia
kuwanufaisha wanawake wapatao 200 kutoka Wilayani Kibaha mkoani Pwani
pamoja na maeneo mengine ya jirani ambao watapatiwa mafunzo mbali mbali
ya ujasiriamali.
No comments :
Post a Comment