Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Napenda
kutumia nafasi hii kwanza kabisa kumshukuru mwenyezi mungu kwa
kuniwezesha kuwa mzima hadi siku hii ya leo. Ni dhahiri kwamba mmekuwa
pamoja tangu nilipochaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Lakini
pia mmekuwa bega kwa bega na mimi Meya wenu
wa Jiji, katika juhudi kubwa
za kulifanya jiji letu kuwa la kuvutia. Hivyo nina kila sababu ya
kuwashukuru na kuwapongeza sana.
Ushirikiano
ambao mnaunyesha na kuendelea kuuonyesha unanipa matumani makubwa
kwamba tuko pamoja katika kuhakikisha kwamba tunaleta mabadiliko makubwa
katika jiji letu na hivyo kuondokana na changamoto mbalimbali zinazo
likabili jiji letu. hivyo naomba tuendelee kushirikiana na kuzidi
kuniombea Meya wenu niweze kufanya kazi ambazo mmenituma katika jiji letu la Dar es Salaam.
Ni
wazi mnafahamu kwamba, maendeleo ya jiji letu hajawezi kuletwa bila ya
nyinyi wannachi kuonyesha ushirikiano kwa viongozi wenu ambao
mmetuchagua kuanzia ngazi za Mitaa, Kata, Halmashauri pamoja na jiji.
Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Halmashauri
ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa na mipango mingi mizuri ambayo
imelenga kuboresha maendeleo ya wananchi wake. Miongoni mwa mambo ambayo
niweka na kuendelea kusimamia ili kuhakikisha kwamba wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanapata huduma mbalimbali za kijamii kwa uhakika.
Ndugu wananch wa Jiji la Dar es Salaam.
Hivi
sasa tunaingia kwenye kipindi cha sikuu ya pasaka. Tunapoungana na
wenzetu Wakristo katika kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, niwaombe wakazi
wa jiji la Dar es Salaam kuendeleza kushirikiana na vyombo vyetu vya
usalama katika suala zima la uimarisha wa usalama wenu.
Vyombo
vya usalama vimekuwa rafiki kwa kipindi chote jambo ambalo limefanya
kupungua kwa matukio ya kiuhalifu ndani ya jiji letu.
Hivyo basi nitoe
rai kwa wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam, kusherehekea siku kuu hii
kwa Amani na utulivu bila kuwepo kwa vurugu zozote. Salamu zangu za upendo katika sikukuu hii ya Pasaka ziwe chachu ya kuendelea kutunza amani katika jiji letu, huku mki hakikisha kwamba kila eneo ambalo watoto wenu watashiriki kwa namna moja ama nyingine kuwe na usalama wa uhakika. Tusijenge utamaduni wakukubali matukio ya kuvunja amani kwenye siku kuu maana hizi ni sherehe sio vita.
Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam,
Mtakubaliana
name kwamba, Siku kuu hii imekuja na neema ya mvua, ukizingatia ni
jambo ambalo tulikuwa tukililia kwa muda mrefu sana ili kuondokana na
hali ya ukame. Napenda kutumia fursa hii kuwataka wale wote ambao wapo
maeneo ya hatarishi (mabondeni), kuanza kuchukua tahadhari mapema kabla
ya kukumbwa na adha ya mafuriko.
Sote
ni mashahidi kwamba, wakati wa mvua kama hizi kumekuwa na madhara
makubwa ambayo hujitokeza kwa wale ambao huishi mabondeni. Hivyo kama
jiji linampango mkakati wa kuboresha miundombinu ya maji ili kuepukana
na adha hii ya mafuriko. lakini basi wakati jiji likiwa kwenye mkakati
huo, tuchukue tahadhari mapema kabla ya kuleta maafa.
Ndugu wananchi wa jiji la Dar es Salaa.
Nimekuwa
katika majukumu mbalimbali ya kitaifa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi
wetu. Nitoe rai kwa wananchi kushirikiana na viongozi mliowachagua ili
kuweza kuwasilisha kero zenu sehemu husika ili mamlaka ziweze kushughulikia kero hizo mapema.
Aidha
Ofisi ya Meya wa jiji imekuwa rafiki kwa wananchi wote katika
kuhakikisha kwamba tunakuwa na Jiji ambalo linajali mahitaji mbalimbali
ya wananchi wake hususani wafanyabiashara wadogowadogo, Bodaboda, Mama
lishe, na makundi mengine mbalimbali.
Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Halikadhalika
pia, napenda kuvipongeza vyombo vyote vya habari kwa mchango mkubwa
ambao mnaonyesha wa kuhabarisha Umma wa wa Tanzania mambo mbalimbali
yanayofanywa na jiji. na
kwamba mmekuwa ni chachu kubwa ya kutangaza shughuli mbalimbali
zinazofanywa na jiji. Niseme tu kwamba jiji la Dar es Salaam, linatambua
mchango wenu mkubwa na kuwaomba muendelee kufanya kazi zenu kwa weledi
mzuri na kwamba tuko pamoja na nyie.
Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Mwisho
kabisa niwatakie maandalizi mema ya sikukuu ya Pasaka ,iwe na heri na
fanaka kwa watu wote, na kwamba mapumziko haya ya siku tatu, muyatumie
kwa kulijenga jiji lenu badala ya kulibomoa.
Mwisho kabisa napenda kuwatakia sikukuu njema
Mungu ibariki Tanzania , mungu libariki jiji la Dar es Salaam.
Imetolewa na Mstahiki Meya wa jiji
…………………….
Isaya Mwita Charles.
No comments :
Post a Comment