Saturday, April 15, 2017

POLISI "YATANGAZA VITA" DHIDI YA WALIOUA ASKARI POLISI, KAMISHNA NSATO ATANGAZA KUANZA KWA OPERESHENI KALI




KAMISHINA wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi la  polisi, Nsato Marijani, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, wakati akitoa tamko kuhusu operesheni itakayoendeshwa na jeshi hilo ya kuwasaka wahalifu waliohusika na mauaji ya Askari nane katika msitu wa Jaribu Mpakani Mkoa wa Pwani juzi. Kushoto ni Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba ''Tunaomba wananchi watusamehe kwa operesheni hii tunayokwenda kuianza, kwani askari wanane ni wengi sana na hatutakuwa na msalie mtume kwa hili, wameanza sisi tunamaliza, na jana ilikuwa ni 8 - 4, lakini tukianza nawaambia mabao yetu yatakuwa ni zaidi yao'';. alisema Marijani Aidha Marijani ametangaza kuwa eneo hilo ni marufuku waendesha pikipiki kupita zaidi ya saa kumi na moja jioni. Kaa nasi  
(KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO BLOG)



Tarehe 11 Aprili, 2017, Mhe. Balozi Wilson Mutaganywa Kajumula Masilingi aliwasilisha hati za utambulisho kwa Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico, Ikulu Katika Jiji la Mexico. Hafla hiyo ilishuhudiwa na Mhe. Luis Videgaray Caso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Mexico na mke wa Mhe. Balozi, Marystella Masilingi. Wakati wa kuwasilisha hati hizo, Mhe. Balozi alipata fursa ya kuongea na Mhe. Rais wa Mexico na kumpa salam kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico akimpokea Mhe. Balozi Wilson M. K. Masilingi, Balozi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mexico. Katikati akitizama ni Mhe. Luis Videgaray Caso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico.
Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico na Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi, Balozi mpya wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, nchini Mexico.
Kutoka kushoto, Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi na Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico; Mke wa Balozi Bi. Marystella E. Masilingi na Mhe. Luis Videgaray, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico.
Mhe. Balozi Wilson M. K. Masilingi na Mke wake Bi. Marystella Masilingi (kulia) na Bi. Swahiba Mndeme, Mkuu wa Utawala wa Ubalozi (kushoto)

No comments :

Post a Comment