Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
TBP, Bw. Sabasaba Moshingi akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Mifuko
ya Uwezeshaji ya Serikali katika maonyesho ya mifuko hiyo
yaliyozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa
Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama
akiwasalimia wananchi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofungua
Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa
Uhuru mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimkabidhi Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma, Bw. Godwin Kunambi (wapili
kushoto) hundi ya Shilingi 1, 469, 358,0 00/= kwa ajili ya vijana
kabla ya kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali
kwenye uwanja wa mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Wanne kushoto
ni Wziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Naibu Wziri wake, Anthony
Mavunde. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini , Christina Mndeme
na watatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa wa Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi, Beng Issa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya
TPB, Noves Moses (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba
Moshingi ( wapili kulia) cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko
ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo
kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. Kushoto ni Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mzee Maarufu wa Dodoma, Job Lusinde baada ya kufungua
maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya serikali kwenye uwanja wa
Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Wengine pichani kutoka kulia ni
Waziri wan chi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, AjiraKazi, Jijana,
ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,
Christina Mndeme na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi, Beng Issa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika
maonyesho ya Mifuko ya Uwezesha Wananchi ya serikali baada ya kufungua
maonyesho hayo kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika
maonyesho ya Mifuko ya Uwezesha Wananchi ya serikali baada ya kufungua
maonyesho hayo kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya
TPB, Noves Moses (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba
Moshingi ( wapili kulia) cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko
ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo
kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofiai
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza wakati alipofungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji
Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18,
2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimkabidhi Meneja wa PPF wa Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael
Christian cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji
Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa
Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimsikilza Bi. Evelyne Mandenje amabaye ni mmoja wa wajasiriamali
walionufaika na mikopo inayotolewa na Benki ya TIB wakati alipotembelea
banda la wasindikaji vyakula kabla ya kufungua Maonyesho ya Mifuko ya
Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma
Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na watumishi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakati
alipotembelea banda la benki hiyo kwenye maonyesho ya Mifuko ya
Uwezeshaji Wananchi ya Serikali aliyoyafungua kwenye uwanja wa Mashujaa
mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakijadili jambo katika maonyesho ya
Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali yaliyofunguliwa na Waziri
Mkuu kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 28, 2017. Kulia ni
Afisa Mwandamizi wa Fedha wa Benki ya TIB, Kenneth Lusesa(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amelitaka Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), lianze kufanya
tathmini ya kisayansi kuhusu manufaa ya Mifuko yote ya uwekezaji nchini
ili ...
kujiridhisha endapo inawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.
Pia amelitaka baraza hilo lifanye
tathmini kuhusu namna ya kuunganisha mifuko hiyo bila ya kuathiri
majukumu ya msingi na mantiki ya kuanzishwa kwake, ili inayofanya kazi
zinazofanana iunganishwe .
Ametoa agizo hilo leo (Jumanne,
Aprili 18, 2017) wakati akifungua maonesho ya mifuko ya uwezeshaji
katika uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma. Amesema uzinduzi wa maonesho
hayo ni fursa nzuri kwa wananchi kuweza kudadisi kuhusu huduma
zitolewazo na Mifuko hiyo na kutoa ushauri, ili kuboresha huduma.
“Lengo ni kuwa na Mifuko
michache, lakini inayobadilisha maisha ya wanufaika, ambao ni wananchi.
Nitafurahi kupata taarifa hiyo kabla au ifikapo Mwezi Mei, 2018,”
amesema.
Aidha, Waziri Mkuu amesema
mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi yanayofanywa na Serikali yanalenga
kuwawezesha Watanzania wengi wafanye shughuli za kujiongezea kipato
bila kusumbuliwa na baadhi ya Watumishi wasio waadilifu.
Ameongeza kuwa “uwezeshaji
wananchi kiuchumi ni jambo ambalo lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM
ya Mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mpango wa Taifa wa
Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2017 – 2020/2021,”.
Amesema kuwawezesha wananchi
kiuchumi, sio ubaguzi wala upendeleo, bali ni jitihada za makusudi za
kuwashirikisha wananchi walio wengi ambao kwa sababu za kihistoria,
wamejikuta wakiwa nje ya mfumo rasmi wa kiuchumi, hivyo kubaki kwenye
hali duni jambo ambalo ni hatari kwa ustawi na usalama wa nchi.
Waziri Mkuu amesema jitihada za
uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizoanza tangu Serikali ya Awamu ya
Kwanza na kuendelezwa na awamu zote zilizofuata, ambapo kwa sasa kuna
mifuko 19 ya kuwezesha wananchi kiuchumi.
Amesema mifuko hiyo imesaidia
upatikanaji wa mitaji kwa wajasiriamali na kupunguza kiwango cha
umaskini nchini. “Hadi kufikia mwaka 2016 Mifuko hiyo kwa pamoja ilikuwa
imetoa mikopo yenye thamani ya sh. trilioni 1.759 kwa wajasiriamali
400,000.
Awali Katibu Mtendaji wa NEEC,
Bi. Beng` Issa alisema maonesho hayo ya siku nne yatawezesha kuwaongezea
wananchi uelewa juu ya shughuli zinazofanywa na mifuko ya uwezeshaji.
Amesema kati ya mifuko 19 ya
uwezeshaji mifuko 13 imeweza kushiriki katika maonesho hayo ya kwanza
kufanyika nchini, ambapo kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Wezesha
wananchi kiuchumi ili kujenga uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda”
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB
Bank PLC, Bw. Sabasaba Moshingi aliyezungumza kwa niaba ya washiriki
alisema madhumuni ya maonesho hayo ni kukuza uelewa juu ya uwepo wa
mifuko ya kuwezesha wananchi kiuchumi na fursa zitolewazo na mifuko
hiyo.
Pia kuhamasisha wananchi juu ya
kujijengea utamaduni wa kujiwekea akiba na kuwekeza katika miradi yenye
kuleta faida pamoja na uanzishwaji na uimarishwaji wa vikundi na miradi
ya kiuchumi ili kuunganisha wananchi na fursa za huduma ya mikopo,
mafunzo na huduma nyingine zinazotolewa na mifuko hiyo.
No comments :
Post a Comment