Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM
Taifa, Mh. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wajumbe wa kamati za siasa
za Matawi hadi Wilaya ya Kusini Unguja, huko katika Ukumbi wa Skuli ya
Makunduchi.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM
Taifa, Mh. Samia Suluhu Hassan, akiweka jiwe la msingi katika Tawi la
CCM Mungoni lililopo katika Jimbo la Paje Wilaya ya Kusini Unguja.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM
Taifa, Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wakikagua Tawi
hilo mara baada ya kuweka jiwe la msingi.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,
Mh. Samia Suluhu Hassan, akitroa maelekezo kwa Mbunge wa Jimbo la
makunduchi Mh. Haji Ameir Haji “Timbe” katika jengo la mradi wa skuli ya maandalizi ya Kajengwa Makunduchi.
Baadhi ya wanachama wa CCM
waliokuja Zanzibar kutembea kwa ajili ya siku kuu ya Pasaka, na
wanachama wenyeji pamoja na Raia wa Kigeni waliokuwa katika harakati za
utalii na wakaamua kujumuika na wana CCM katika Tawi la Mungoni.
………………………..
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,
Mh.Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi na watendaji wa chama hicho
kuchukua hatua za kuwasilisha changamoto zinazowabili wananchi kwa
viongozi wa serikali wakiwemo Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu wakuu
na
Wakurugenzi ili watafute ufumbuzi wa kudumu.
Agizo hilo amelitoa wakati
akizungumza na Wajumbe wa Kamati za Siasa za matawi hadi Wilaya za
Wilaya ya Kusini Unguja huko katika Ukumbi wa Skuli ya Makunduchi
alisema baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM wamekuwa na utamaduni wa
kulalamika pindi wanapokutana na viongozi wa ngazi za juu za chama, hali
ya kuwa utatuzi wa kero hizo upo katika uwezo wa utekelezaji wa
viongozi wa serikali wanaotokana na chama hicho.
Maelekezo hayo yamekuja mara baada
ya Katibu wa CCM Wilaya ya Kusini, Hamdan Haji Machano kusoma taarifa
ya utekelezaji na hali ya kisiasa ndani ya Wilaya hiyo iliyokuwa na kero
za Kesi za udhalilishaji wa kijinsia kuwa na urasimu wa kutotolewa
hukumu haraka, pamoja na upungufu wa maji safi na salama kwa baadhi ya
maeneo.
Mh. Samia ambaye pia ni Makamo wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alieleza kwamba tabia hiyo
inatakiwa kukemewa kwani haijengi uimara wa chama, kwani inatoa mwanya
wa viongozi wa Chama kuwaogopa watendaji wa Serikali wakati wao ndio
waliowapa ridhaa ya kuongoza dola.
Alisema haiwezekani wananchi
wakabiliwe na changamoto za kijamii, kisiasa na kiuchumi wakati wapo
viongozi wa serikali wenye dhamana ya kutatua kero hizo.
Akifafanua juu ya Changamoto ya
vitendo vya ubakaji na udhalilishaji wa Kijinsia, Mh. Samia aliwambia
viongozi hao kuwa suala hilo walipeleke kwa Waziri anayehusika na
masuala ya Katiba na Sheria ili aweze kuwasimamia watendaji wake
watekeleze wajibu wao.
“Nyingi ndio mabosi wa hao
viongozi wote waliopo serikali haiwezekani eti serikali mmeiweka
madarakani alafu mnakuja kukaa wanyonge kwa kuwa kuna matatizo
yanawakabili wananchi yamekosa utekelezaji kutokana na Urasimu wa
viongozi wachache, na mkiwaita wakakataa kuja nendeni kwa Rais wa
Zanzibar Dkt, Shein ambaye ni Makamo Mwenyekiti wa Chama chetu.
Lazima tuwe imara na misimamo
thabiti ya kiutendaji ndani na nje ya chama chetu kwa kuondokana na
uendeshaji wa taasisi yetu kwa mazoea kwani sote tupo kwa ajili ya
wananchi ”, Alisema Mh.Samia.
Alifafanua Mh.Samia na kuongeza
kwamba CCM mpya na Tanzania mpya ni muhimu dhana hiyo kutekelezwa kwa
vitendo ili kuendana na marekebisho ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977
yaliyofanyika hivi karibuni, kwa lengo la kuongeza ufanisi ndani ya
taasisi hiyo.
Hata hivyo aliwataka wanachama wa
CCM hasa vijana kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi katika
Uchaguzi wa Chama unaoendelea kwa sasa katika ngazi za mashina na matawi
huku akiwasihi Wazee kuwa karibu na vijana wao sambamba na kuwafunza
uzalendo na itikadi za chama hicho.
Alisema Chama hicho kwa sasa
kinaenda na kasi ya kiutendaji na kiungozi isiyokuwa ya kawaida ambayo
ameifananisha na kasi ya mtandao wa 4G, hivyo panahitajika nguvu za
vijana imara walioiva kiuzalendo ambao wataweza kupokea kijiti cha
uongozi kutoka kwa wazee waliotumikia nchi na chama kwa muda mrefu.
“ Vijana mtakapokaa kando basi
jueni hii nchi mtaiuza kwa gharama nafuu na kuirudisha itakuwa ni
vigumu, lazima mtulie na kuacha tabia za kukubali kushawishiwa na kuweni
na msimamo ili mjenge heshima kwa vizazi vyenu vya sasa na baadae ,
kama ilivyo kwa wazee wetu waliokomboa Tanzania bara na Zanzibar na kwa
sasa tunafaidi matunda yao.”, Alisisitiza mwanasiasa huyo.
Pamoja na hayo alisisitiza umuhimu
wa wachama, watumishi na viongozi wa jumuiya na chama kusoma kwa kina
Katiba ya Chama na kanuni zake ili waweze kujua majukumu yao ili
wajadili changamoto na kuzipatia ufumbuzi kwa njia ya vikao rasmi vya
kikanuni.
Hata hivyo Kabla ya kuwahutubia
Wanachama hao alianza kufanya kazi za uimarishaji wa Chama kwa kuweka
jiwe la msingi katika Tawi la kisasa la Mungoni Jimbo la Paje, sambamba
na kutembelea miradi ya ujenzi wa skuli mbili zenye ukumbi wa mikutano
iliyogharimu kiasi cha zaidi ya milioni 217, katika vijiji vya Kajengwa
na Kizimkazi ambazo ni moja ya ahadi alizotoa wakati akiwa na nafasi ya
Ubunge katika jimbo la Makunduchi.
Mapema akizunguimza katika kikao
hicho, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadalla “
Mabodi” aliwambia viongozi hao kwamba mtaji wa chama kisiasa ni
wanachama hai wanaokubalika kisheria, hivyo kila mtu anatakiwa kutendea
haki nafasi aliyokuwa nayo ili chama hicho kishinde katika uchaguzi wa
2020.
Dkt.Mabodi aliwasihi wanachama hao
kuwachagua viongozi wenye ushawishi na wanaokubalika katika jamii
watakaoweza kuongeza wanachama wapya kutokana hata katika vyama vya
upinzani, na makundi mengine yaliyopo nchini.
Pia aliahidi kwamba atatumia uwezo
na ujasiri wake katika kusimamia masuala ya kiutendaji ndani ya chama
ili kwenda sambamba na matarajio, dira na dhamira ya Chama hicho kwa
kuwatumikia wananchi kwa weledi.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi katika harakati za ziara hiyo kabla ya kuanza kwa kikao hicho
mmoja wa Raia Swaziland wanayeishi hapa nchini Bw. Nicolas Sarraj
amesifu siasa zinazofanywa na CCM, zilizozaa matunda ya kuwepo kwa sekta
ya utalii ambayo imetoa uhuru wa raia wan chi za kigeni kuja nchini
kutalii kwa amani na Utulivu.
Sambamba na hayo alisema Zanzibar
imekuwa kitovu cha maendeleo katika ukuaji wa sekta mbali mbali za
miundombinu zikiwemo barabara, viwanja vya ndege pamoja na uimarishaji
wa huduma za kijamii na kiuchumi.
No comments :
Post a Comment