Mwakilishi wa mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Sigisbert Rwezaula akizungumza
katika hafla ya kupongeza shule za msingi kumi bora kwa mtihani wa taifa
wa mwaka 2016
Afisa Elimu Msingi Wilaya, Sosthenes Mbwilo akitambulisha walimu na waratibu elimu kata katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi, Sigisbert Rwezaula
akitoa cheti kwa mmoja wa walimu wakuu wa shule zilizofanya vizuri.
Wengine pichani kulia ni Afisa Ugavi Wilaya, George Ngwesa.
Walimu wakifurahia cheti walichopewa kwa kutambua kufanya vizuri kwa shule yao.
Wageni waalikwa wakiserebuka muziki ikiwa ni moja ya shamrashara za kupongezana kwa kazi nzuri.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na walimu wakuu wa shule kumi bora pamoja na maofisa elimu mbalimbali.
Mwakilishi wa mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Sigisbert Rwezaula akizungumza
katika hafla ya kupongeza shule za msingi kumi bora kwa mtihani wa taifa
wa mwaka 2016. . Wengine pichani kuanzia kushoto ni Afisa Ugavi Wilaya,
George Ngwesa, Afisa Elimu Msingi Wilaya, Sosthenes Mbwilo na Katibu wa
Tume ya Utumishi wa
Walimu (TSC), Paul Sheka.
Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu mkoani Shinyanga wamepongezwa kazi nzuri na kupata matokeo
mazuri ya shule zao za msingi katika mtihani wa taifa wa mwaka jana.
Pongezi hizo zilitolewa jana na
mwakilishi wa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Sigisbert
Rwezaula wakati wakati wa hafla ya kupongeza shule kumi zilizofanya
vizuri katika mitihani ya mwaka jana.
Katika hafla hiyo iliyofanyika
Mwadui wilayani Kishapu ikiambatana na utoaji vyeti kwa walimu wakuu,
Rwezaula ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema hakuna muujiza wa kufanya
vizuri bali ni walimu kujituma.
Aliwataka walimu wakuu wa shule
ambazo hazikufanya vizuri kuhakikisha wanaweka mikakati ili ziweze
kuibuka vinara kama walivyo wenzao na kuwataka kuendelea kujituma.
”Najua kuna changamoto nyingi kwa
walimu kama upungufu au ukosefu wa fedha lakini nawaomba tuvumilie na
tukabiliane nazo, jambo kubwa ni kutoa elimu bora kwa wanafunzi wetu na
hatimaye wafanye vizuri,” alisisitiza.
Aidha Rwezaula aliongeza kwa kutoa
rai kwa walimu wa shule hizo za msingi zilizopo katika halmashauri hiyo
kuwa na utamaduni wa kujiendeleza kimasomo ili kukabiliana na
changamoto mbalimbali.
Alisema hivi sasa dunia ipo katika
utandawazi ambapo kunashuhudiwa ugunduzi mkubwa wa kiteknolojia ambao
unahitaji maarifa makubwa ili kuendesha masuala mbalimbali ya kitaaluma.
”Ni vizuri walimu mkajiendeleza
kielimu msiishe hapo mlipo, msikubali kuwa nyuma ya wakati kwani hivi
sasa elimu ni muhimu sana na mnashuhudia dunia ni kama kijiji mnaweza
kupata habari kwa mitandao,” alisema.
Rwezaula aliwataka kuwa na
utaratibu wa kufidia vipindi vilivyopotea wakati mwalimu kapata dharura
au ruhusa na kushindwa kuingia darasani na kuwafundisha wanafunzi.
Alisema kwa kuwa na utaratibu huo
kutawawezesha wanafunzi kupata wasaa wa kujifunza na kuelewa masomo yao
kwa wakati na hivyo kufanya vizuri zaidi kwenye mitihani yao.
Awali wanataaluma hao walifanya
kikao kazi cha kutathmini mambo yaliyojiri kitaaluma katika Idara ya
Elimu Msingi halmashauri ya wilaya hiyo kipindi cha mwaka 2016.
Kikao hicho kilichofanyika Mwadui
kilihusisha maofisa elimu msingi, waratibu elimu kata, walimu wakuu na
badhi ya walimu wa shule mbalimbali za msingi zilizopo Wilaya ya Kishapu
No comments :
Post a Comment