Sunday, April 2, 2017

BREAK NEWS,CHADEMA YAPATA PIGO MUHEZA MWENYEKITI WA WILAYA HIYO AJIUNGA NA CCM

 
IMG_7290
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama
hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha akizungumza na
waandishi wa habari mapema leo kutangaza azma ya kuondoka Chadema na
kuhamia CCM 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Mkoani Tanga kimepata pigo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa
chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha kuamua

kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM)
leo kutokana na chama hicho kupoteza dira na
mwelekeo.



Lakini kubwa zaidi inatokana na mambo yanayofanywa na chama hicho kwa
kuiondoa uhalisi wa chama hicho ambayo wananchi walikuwa wanaitegemea
kuwa chama cha kuwa mshindani na CCM ili kuleta
mabadiliko.



Hatua ya mwenyekiti huyo kutangaza kujiuzulu inakuja siku chache baada
ya maamuzi wa mkutano mkuu wa viongozi wa chama kanda ya kaskazini mjini
Tanga uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kuridhia
kuvunja uongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya ya mkoa wa
Tanga.



Akitangaza uamuzi huo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari
uliofanyika leo kwenye ukumbi wa BMK uliopo Sahare Jijini
Tanga,Rwebangira Karuwasha alisema hayo ndio mambo makubwa yaliyopelekea
kuamua kukaa pembeni na kujiunga na CCM ambako anaona kuna sera makini
zinazotekelezeka .



Alisema kutokana na matukio mbalimbali anayoyafanya Mwenyekiti wa Chama
hicho Taifa, Freeman Mbowe sitegemei kuendelea kubaki kwenye chama hiki
cha watumwa  na watwana hivyo nimeamua kujiunga na CCM kwani ndio chama
kinachoweza kutekeleza sera makini na zenye
mafanikio.



“Kwa mfumo wa uongozi unaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema
Freeman Mbowe haukubaliki na hakuweza kuvumilia…. sitegemei kuendele
kuwepo kwenye chama hicho kilichokuwa cha watwana na watumwa hivyo
nimeridhia kujiunga na CCM “Alisema.


“Kuanzia leo mimi sio mwanachama wa Chadema  na nitajiungha na CCM ya
sasa chini ya Rais Dokta John  Magufuli sababu Chadema wameacha sera na
makini kwa ajili ya kuwapa maendeleo wananchi.



Alisema pia sababu nyengine ni kutokana na utendaji wa Rais
John

Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambao umekuwa mstari
wa mbelea kujali wanyonge na kusaidia harakati za kimaendeleo hapa
nchini.



Aidha alisema wameshindwa kuelewa kuwa Mwenyekiti Mbowe alipangua gia
angani kumuondoa dkta Slaa wakati alipokuwa kwenye chama hicho jambo
ambalo ni hatari kwa ukuaji wa chama hicho.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments :

Post a Comment