Na Jumia Travel Tanzania
Ni mara
ngapi umeshawahi kusikia ofa mbalimbali za mtangazo ya biashara kupitia
vyombo vya habari? Je huwa unashawishika au kuvutiwa nayo mpaka
kukupelekea kununua?

Kutoa
punguzo la bei ni njia ya haraka zaidi inayotumiwa na wafanyabiashara
wengi kuwavutia wateja. Tafiti zinaonyesha umakini wa mteja na ushawishi
katika kutumia huduma fulani huja kwa ofa au punguzo la bei. Muda
wowote ambao utamwambia mteja kwamba anaweza kuokoa pesa, ipo asilimia
kubwa ya kuteka umakini wake na kukusikiliza.
Zipo
sababu kadhaa zinazowafanya wafanyabiashara kutoa matangazo ya punguzo
katika bidhaa na huduma zao. Sababu hizo zinaweza kuwa kama vile
kuwavutia wateja, kuongeza mauzo, kupunguza hifadhi ya bidhaa
zisizohitajika dukani, kujijengea jina, kufikia malengo ya kibiashara,
na kuokoa gharama nyinginezo za kuendesha biashara.
Tukielekea
msimu wa mapumziko ya sikukuu za Pasaka tunaamini utayasikia matangazo
ya kila aina yanayokushawishi kutumia huduma fulani. Huduma kama vile za
usafiri, mavazi, malazi, samani na kadhalika ni miongoni mwa
zitakazokuwa kwenye mzunguko wa vyombo mbalimbali vya habari kukuvutia
wewe mteja.
Jumia
Travel inaamini kwamba sio watu wote ambao wanatumia ofa hizi ambazo
hutangazwa mara nyingi kwenye misimu ya sikukuu kama hii ya Pasaka
ambayo inakuja. Inawezekana kukawa na sababu za mtu kuamua kutotumia ofa
hizo lakini kuna manufaa mengi tu kama vile:

Kuokoa
gharama za matumizi yako ya kawaida. Ni kweli kabisa endapo utakuwa
ukifanya manunuzi yako kipindi cha ofa utakuwa unafaulu katika hili.
Kipindi pekee ambacho huwa na ofa nyingi ni cha sikukuu na mwisho wa
mwaka. Na ni kutokana na uhitaji mkubwa kutoka kwa wateja kwa wakati huo
ndio unaowalazimu kufanya manunuzi makubwa.
Lakini
pia ofa hurahisisha mahitaji yako kama mteja. Kupitia punguzo la bei
unaweza kukuta pesa ambayo ilibidi ununue bidhaa moja unaweza kuongezea
na zingine. Hivyo hapo utakuwa umerahisisha mahitaji yako kwa kutumia
kiasi kilekile bila ya nyongeza yoyote.

Kwa hali
ya maisha ya sasa inabidi mtu kuwa makini sana na namna unavyotumia pesa
kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Umakini huo ni pamoja na kufuatilia
kwa ukaribu ili kuendana na tabia za wafanyabiashara na soko kwa ujumla.
Fuatilia
kujua ni kipindi gani bei za bidhaa na huduma huwa ni za gharama ya juu
na ni wakati gani hushuka. Kwa mfano, itakuwa haina maana kununua
luninga kwa bei fulani wakati unaweza kuipata kwa nusu bei kipindi cha
ofa.
Kwa
wafanyabiashara wengi nchini na duniani kote kwa ujumla, hutoa ofa za
bidhaa na huduma hasa kipindi cha sikukuu na mwisho wa mwaka. Kwa sababu
kipindi hiko uhitaji miongoni mwa wateja huwa ni mkubwa na wako radhi
kununua bidhaa au kutumia huduma.
Jaribu
kuanza kufuata utaratibu huu kuanzia sasa na uone ni kwa namna gani
utakuwa na manufaa kwako. Mwaka bado mbichi, zipo sikukuu kadhaa
zinakuja siku za usoni. Jaribu kutembelea Jumia Travel ujionee ofa
zilizotolewa na hoteli mbalimbali kwa ajili ya msimu huu wa sikukuu.
No comments :
Post a Comment