Waziri wa Afya Mahmoud Thabit
Kombo akizungumza na waandishi wa habari juu ya kufanyika Kongamano la
Kimataifa la maradhi ya vichwa maji, uti wa mgongo na kensa ya ubongo
litakaloanza kesho katika kituo cha Neurosurgical Mnazimmoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya
Dkt. Jamala Adam Taib (kushoto) na Dkt. Mahmoud Quresh wakimsikiliza
Waziri wa Afya (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari kituo cha NED Mnazimmoja.
Dkt. Mahmoud Quresh anaesimamia
upasuaji wa maradhi ya vichwa maji, uti wa mgongo na kensa ya ubongo
katika wodi ya maradhi hayo Hospitali ya Mnazimmoja akitoa ufafanuzi wa
masuala ya waandishi wa habari kuhusu kufanyika Kongamano hilo Zanzibar.
Mwandishi wa habari mwandamizi wa
Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhani Ali akiuliza swali katika
mkutano wa waandishi uliofanyika kituo cha NED Mnazimmoja.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
…………………….
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
Zanzibar itakuwa mwenyeji wa
Kongamano la Kimataifa la maradhi ya vichwa maji na uti wa mgongo na
kensa ya ubongo litakalofanyika kwa siku tatu kuanzia kesho katika kituo
cha
maradhi hayo Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari
katika kituo cha upasuaji wa maradhi hayo NED, Waziri wa Afya Mahmoud
Thabit Kombo alisema nchi tisa kutoka Afrika, Ulaya na Marekani
zitashiriki Kongamano hilo.
Amesema Zanzibar imepewa nafasi
hiyo kutokana na juhudi za Rais Shein katika masuala ya elimu na utafiti
pamoja na ubora wa kituo hicho na utulivu wa wananchi.
Waziri Mahmoud ameongeza kuwa
tokea kuanzishwa kituo hicho miaka miwili iliyopita zaidi ya wananchi
600 kutoka ndani na nje ya Zanzibar wamefanyiwa upasuaji ambapo
asimilimia 92 zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Amesema kuwepo kwa kituo hicho
Zanzibar kimeipunguzia Serikali mzigo wa kutumia fedha nyingi
kuwapeleka nje wagonjwa wanaokabiliwa na matatizo hayo ambapo gharma
zake ni zaidi ya shilingi milioni 12 kwa mgonjwa mmoja.
Ameeleza kuwa kongamano hilo
litakalosimamiwa na Daktari bingwa wa maradhi ya vichwa maji, uti wa
mgongo na kensa ya ubongo kutoka Marekani Professa Paul Young litakuwa
ni fursa pekee kwa madaktari wa Hospitali za Serikali na za watu binafsi
kujifunza njia bora za kutibu maradhi ya hayo.
Akieleza malengo ya baadae ya
Serikali ya kituo hicho Waziri Mahmoud Thabit Kombo alisema ni kufungua
tawi Pemba na kukifanya kuwa kituo kikuu kwa nchi za Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya
Dkt. Jamala Adam Taib alisema juhudi zinaendelea kusomesha madaktari
wazalendo wa kada mbali mbali ikiwemo maradhi ya vichwa maji, uti wa
mgongo na mishipa ya fahamu ili kupata madaktari wa kutosha
watakaoendesha kituo hicho baada ya kuondoka wataalamu wa kigeni waliopo
hivi sasa.
No comments :
Post a Comment