Wednesday, March 29, 2017

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAFANYA MAPITIO YA BAJETI YAKE MJINI DODOMA KABLA YA VIKAO VYA BUNGE LA BAJETI KUANZA


 D
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  akitoa Maelekezo kwa  Watendaji Wakuu wa  Wizara yake wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni sehemu ya maandalizi  muhimu  kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kushoto ni  Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
D 1
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  akiwa pamoja na Watendaji Wakuu wa  Wizara yake wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni sehemu ya maandalizi  muhimu  kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, wa kwanza kulia ni Naibu  Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Massauni  na wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo, Balozi  Hassan Simba Yahaya, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
D 2
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakipitia bajeti za taasisi zao,  ikiwa ni sehemu ya maandalizi  muhimu  kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa [NIDA] Massawe, akifuatiwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.  Anna Peter Makakala, watatu kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye na wanne ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Dr. Juma Malewa. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
D 3
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba  akiwa pamoja na  Watendaji Wakuu wa  Wizara yake wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni sehemu ya maandalizi  muhimu  kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
D 4
Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,  wakipitia bajeti zao, wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni sehemu ya maandalizi  muhimu  kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
D 5
Baadhi ya Makamishna wa Uhamiaji, Magereza, na Zimamoto na Uokoaji pichani,  wakipitia bajeti zao, wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti  ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni sehemu ya maandalizi  muhimu  kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. [PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YANCHI]
 
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments :

Post a Comment