Picha ya pamoja ya mawaziri wa
jumuiya ya umoja wa Afrika Mashariki Mara baada ya ufunguzi wa Kongamano
LA kupanga jinsi ya kukabiliana na majanga.Kongamano hilo lilizinduliwa
na Rais Pierre Nkurunzinza
Mganga Mkuu wa Serikali toka
Tanzania (wa kwanza kushoto) Prof.Bakari Kambi akichangia mada katika
mkutano huo uliokutanisha wadau wa afya kutoka Afrika mashariki.
Baadhi ya wajumbe toka Kenya wakifuatilia mada zilizowasilisha kwenye mkutano huo.
…………….
Bujumbura,Burundi
Nchi wanachama wa Umoja wa Afika
mashariki pamoja na sektarieti ya umoja huo(EAC) wamehimizwa kuharakisha
mchakato wa kuhakikisha kada zingine za afya ikiwemo ya uuguzi
na kada
nyingine zenye sifa na viwango vinavyofanana na madaktari kuajiriwa
kwenye nchi yeyote ya Afrika Mashariki
Hayo yamesemwa jana na Waziri WA
Afya,Maedeleo ya Jamiii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni
Mwenyekiti wa Baraza la Kisekta la mawaziri wa Afya wa Afrika mashariki
kwenye kikao cha 14 nchini hapa
Waziri ummy alisema amefurahishwa
sana na hatua iliyofikiwa na nchi wanachama wa Jumuiaya hiyo ambapo
hivi sasas madaktari wanaotoka katika jumuiya hiyo kuajiriwa
Katika hatua nyingine kikao hivho
kimejadili kuhusu kuimarishwa kwa mafunzo na usimamizi wa pamoja wa
waraalam wa afya,udhibiti wa magonjwa ya milipuko pamoja na magonjwa ya
kuambukiza kama vile Ebola,Mafua makali ya ndege kifua kikuu(TB) na
UKIMWI
Kuhusu kupunguza vifo vya wanawake
wajawazito na watoto ,mawaziri wamekubaliana hao wamekubaliana kuongeza
juhudi Zaidi ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto ndani
ya Afrika Mashariki
“Bado Afrika Mashariki hatufanyi
vizuri katika afya ya uzazi na mtoto na hivyo kusababisha kutofikia
malengo ya kidunia ya Millenia yaliyowekwa,hivyo tuongeze jitihada
katika hili”,alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy ameelekeza Tume
ya Utafiti wa masuala ya Afya ya EAC ihamie mapema makao makuu yake
mjini hapa kama ilivyokubaliwa kwenye vikao vya baraza la mawaziri
vilivyotangulia
Wakati huo huo Waziri Ummy
akiwa nchini humo ameshiriki uzinduzi wa kongamano la Kimataifa la afya
ya Sayansi lililofunguliwa na Rais wa Burundi Mhe.Piere Nkurunzinza
ambalo limeandaliwa na Kamisheni ya Utafiti wa Masuala ya Afya ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kongamano hilo la siku tatu lina
lengo la kujadili na kujipanga katika kukabiliana na majanga ikiwemo ya
magonjwa mapya yanayojitokeza(Emerging Diseases) na yale yanayojirudia
(Re-emerging Diseases) na linawawashirikisha wataalam wa afya na
watafiti kutoka nchi mbalimbali.
No comments :
Post a Comment