Faida ya Hifadhi endelevu ya
Mazingira. Pichani ni eneo la Ngaresero Wilaya ya Meru ambapo kuna
uhifadhi mzuri wa mazingira. Hata hivyo eneo hilo limeanza kuvamiwa na
wananchi kwa shughuli za kibinadamu na kuhatarisha uhai wake. Waziri
Makamba ametembelea eneo hilo na kumtaka Bw. Timoth Leach mmiliki wa
Ngaresero Mountain Lodge kufanya ukaguzi wa mazingira mara moja ili
kubaina matumizi sahihi ya rasilimali maji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipanda mti wa
kumbukumbu nyumbani kwa Hayati Edward Moringe Sokoine. Waziri Makamba
yuko katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha na alitembelea msitu wa
Enguiki na Lendikinya kisha alizungumza na wananchi katika mkutano wa
hadhara.
No comments :
Post a Comment