Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Uongozi wa
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kutembelea eneo hilo
kujionea changamoto za kimazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Baraza la
wafugaji (hawapo pichani) katika Wilaya ya Ngorongoro. Wafugaji hao
walimweleza Waziri kilio cha muda mrefu cha mradi wa Josho Wilayani
hapo, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Ngorongoro na Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kuleta ufumbuzi mapema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Uongozi wa
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kutembelea eneo hilo
kujionea changamoto za kimazingira.
……………..
Na Lulu Mussa,Ngorongoro
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira nchini Mhe. January
Makamba amesema kuwa ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili
kudhibiti
mimea inayohatarisha uoto wa asili katika Mamlaka ya Ngorongoro.
Katika kutatua changamoto hii,
Waziri Makamba ameagiza kuundwa kwa jopo la wataalamu kutoka Tume ya
Sayansi na Tecknolojia, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira, Hifadhi za Taifa za Tanzania, Wizara ya Kilimo na Mifugo na
Mamlaka ya Ngorongoro ndani ya miezi sita kufanyika kwa utafiti wa kina
wa kisayansi wa kubaini mbinu mpya ya kupambana na mimea hiyo vamizi
inayotawala mimea inayotumiwa na wanyama.
Akizungumza katika kikao
kilichojumisha Wahifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro na Wajumbe wa Baraza
la wafugaji, Waziri Makamba amesikitishwa na kitendo cha Uongozi wa
Mamlaka ya Ngorongoro kushindwa kuandaa mpango kabambe wa usimamizi wa
hifadhi baada ya ule wa awali kuisha muda wake. Waziri Makamba ameuagiza
uongozi wa Ngorongoro kuandaa mpango huo mapema na kuwa shirikishi. ”
Mpango mtakoandaa hakikisheni kuwa unakuwa shirikishi kwa jamii
inayozunguka na wadau na Taasisi muhimu likiwemo Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Waziri Makamba pia ameagiza
kufanyika kwa ukaguzi wa kimkakati wa Mazingira utakaojumuisha Wilaya
nzima ya Ngorongoro na kuitaka Mamlaka ya Ngorongoro kushirikiana na
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kutekeleza
wajibu huo mapema. Ukaguzi huo wa kimkakati wa kimazingira kwa Wilaya
hiyo unatazamiwa kutoa mtazamo wa hali ya mazingira kwa miaka hamsini
ijayo.
Aidha, Waziri Makamba ameagiza
kufanyika kwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira ama Ukaguzi wa
Mazingira katika Hotel zote zilizopo eneo la hilo na kulitaka Baraza la
Taifa la Hofadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupita siku ya
Alhamisi tarehe 30/03/2016 kuwaandikia adhabu na kuwatoza faini
wahusika wote ambao hawana vyeti hivyo. “Haiwezekani toka mwaka 2004
Sheria ipo na mpaka leo watu wanaendea na mchakato, hii haikubaliki!”
Alisisitiza Makamba.
Katika hatua nyingine Waziri
Makamba ametoa miezi sita kwa wamiliki wa Hotel zilizopo katika Mamlaka
ya Ngorongoro kuwekeza katika mfumo mpya wa kuvuta maji kutoka Mto
Lukusale na kusitisha mfumo wa sasa wa kutoa maji kwenye creator.
Pia Makamba ameutaka ungozi wa Mamlaka ya Ngorongoro ndani ya miezi
sita kuandaa ramani itakayoonyesha mito na vijito vyote vilivyopo ndani
ya hifadhi hiyo.
Waziri Makamba ametoa maagizo hayo leo juu ya namna bora ya kutumia rasilimali ya “creater”
kwa ajili ya utalii na Uhifadhi wa Mazingira, ikiwa ni pamoja na
utekelezaji wa zuio la mifugo ndani ya crater. Ziara maalumu na mahsusi
ya kukagua utekelezaji na uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira
inayofanywa na Waziri Makamba hii leo imefika Wilayani Ngorongoro.
No comments :
Post a Comment