Mwenyekiti wa Bodi DKT.Ambwene Mwakyusa, akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mkutano
wa Mashauriano baina ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi, Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini
DPP, unafanyika kwa siku mbili kuanzia jana, Rock City Mall Jijini
Mwanza.
Judith Ferdinand, BMG
Jeshi la Polisi nchini limehimizwa kuwaruhusu na kuwawezesha wataalamu katika fani ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi waliosajiliwa, kuhudhuria mafunzo mbalimbali yanayoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi.
Jeshi la Polisi nchini limehimizwa kuwaruhusu na kuwawezesha wataalamu katika fani ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi waliosajiliwa, kuhudhuria mafunzo mbalimbali yanayoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi.
Wito
huo ulitolewa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wabunifu Majengo
Dkt.Ambwene Mwakyusa, katika ufunguzi wa mkutano wa mashauriano kati ya
Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la
Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka Biswalo Mganga, uliofanyika kwenye
ukumbi wa Rocky City Mall.
Dkt.Mwakyusa
alisema, mafunzo hayo endelevu yanayoandaliwa na Bodi hiyo mara mbili
kwa mwaka yanalengo la kuwaelimisha wataalamu hao,ili waendane na kasi
ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia sambamba na kukabiliana na
changamoto.
“Tunatambua
jeshi la polisi lina wataalamu katika fani za ubunifu majengo na
ukadiriaji majenzi waliosajiliwa na ambao hawajasajiliwa na bodi, hivyo
naomba liendelee kuwaruhusu na kuwahimiza wataalamu hao, ili waweze
kusajiliwa,” alisema Mwakyusa.
Hata
hivyo alisema, kwa mujibu wa Sheria namba 4 ya mwaka 2010, Bodi
inamajukumu ya kusajili na kuratibu mienendo ya Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi na wataalamu wanaoshabiana ambopo mpaka mwaka 2016
imesajili wataalamu 1442 na makampuni 393 pamoja na kukagua miradi ya
ujenzi kwa lengo la kuhakikisha imebuniwa na inasimamiwa na wataalamu
waliosajiliwa na Bodi.
Aidha
alisema, kwa mwaka 2016/ 2017 Bodi imepanga kukagua miradi 1800 nchi
nzima,ambapo hadi kufikia mwaka jana jumla ya miradi 1227 imekaguliwa
sawa na asilimia 68 ya lengo,huku hatua mbalimbali zilichukuliwa kwa
miradi iliyokuika sheria ikiwa ni pamoja na kusimamisha shughuli za
ujenzi na kufungua mashtaka mahakamani.
Pia
aliliomba Jeshi la Polisi kufuata taratibu za ujenzi katika ubunifu na
usimamizi wa majengo ya jeshi hilo,ikiwa ni pamoja na kutumia makampuni
ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi,kama sheria namba 4 ya mwaka
2010 inavyotaka,hivyo itasaidia kuhamasisha jamii kutii sheria za nchi.
Kamishna wa Polisi (Oparesheni na Mafunzo), Nsato Marijani akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi Jijini Mwanza.
Kamishina
wa Polisi na Oparesheni na Mafunzo, Nsato Marijani, alisema,
wataendelea kuwatumia Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi ,ambao ni
watumishi wa Jeshi la Polisi na kuwaendeleza wale ambao hawajasajiliwa
na Bodi, ili wawe na sifa za kusajiliwa.
Alisema
jeshi hilo litaendelea kuwatumia kuwatumia wahandisi na makandarasi
waliosajiliwa katika ujenzi wa makazi na ofisi za askari, kwani kwa
kufanya hivyo jamii haitaona ajabu pale watakapo wachukulia hatua za
kisheria wale ambao wanajenga bila kutumia wataalamu.
No comments :
Post a Comment