Na : Mwandishi Wetu
Mamalaka ya Hali ya Hewa nchini
(TMA) imewashauri wananchi na Mamlaka za Miji kuhakikisha kuwa mifumo
na njia za kupitisha maji katika maeneo yao inafanyakazi kwa
kiwango cha
kutosha ili kuepuka madhara yanayowezo kutokana na mvua za msimu
zinazotarajiwa kuanza Mwezi Machi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya
Hali ya Hewa nchini (TMA) Dkt. Agnes Kijazi ametoa kauli hiyo leo jijini
Dar es salam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwelekeo
wa msimu wa mvua Tanzania katika kipindi cha mvua za masika kuanzia
Machi hadi Mei.
Amesema kuwa yapo maeneo ambayo
yatapata mvua za wastani na juu ya wastani na wengine chini ya wastani
ni vema wananchi wakachukua tahadhari ili kuepuka madhara mbalimbali
ambayo yanaweza kuwapata kutokana na mvua hizo.
Dkt. Kijazi ameongeza kuwa mvua
hizo zinaweza kusababisha maji kutuwama katika baadhi ya maeneo ya hivyo
kusababisha mafuriko ambayo yatapelekea kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko
na uharibifu wa miundombinu mbalimbali ikiwemo mifumo ya maji na
barabara.
Aidha ,Mkurugenzi Mkuu amesema
kuwa hali ya unyevunyevu katika udongo inatarajiwa kuimarika kiasi cha
uzalishaji wa malisho ya mifugo na ukuaji wa mazao katika baadhi ya
maeneo kuongezeka .
Hata hivyo , Mkurugenzi Mkuu huyo
amewashauri wafugaji kuwa na mifugo ambayo inalingana na uwezo wa
malisho yaliyopo kulingana na ushauri wa Maafisa Mifugo.
Vile vile ameshauri wananchi
kuzingatia taratibu za uvunaji , uhifadhi na matumizi endelevu ya
rasilimali ya maji katika maeneo ambayo yatapata mvua za wastani na
chini ya wastani ili kuwa na hifadhi ya kutosha ya maji kwa ajili ya
matumizi ya baadaye wakati wa shida ya maji.
Dkt. Kijazi alimeyataja maeneo
ambayo yanatarajiwa kuwa mvua ya wastani na juu ya wastani kuwa ni
Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi, Mbeya na Iringa.
Maeneo ambayo yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani ni njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, na kusini mwa Morogoro.
Amesema kuwa ukanda wa Ziwa
Victoria na maeneo ya pwani ya Kaskazini mvua zinazoendelea kunyesha
zinatarajiwa kuungana na msimu wa Machi na kusambaa katika maeneo
mengine.
Dkt. Kijazi amesema kuwa maeneo
ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro , Tanga, Dar es Salaam, Kaskazini mwa
Morogoro na Visiwa vya Unguja na Pemba yanatarajiwa kuwa na mvua za
chini ya wastani na vipindi virefu vya ukavu.
No comments :
Post a Comment