Monday, March 27, 2017

TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO NA HABARI KUCHOCHEA AZMA YA TANZANIA KUWA NCHI YA UCHUMI WA KATI.


tek1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete(katika) akitembelea maeneo ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) alipokuwa mgeni rasmi katika halfa ya kuzindua Kozi mpya za Masomo International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchn.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa NIT, Profesa Blasius Nyichomba  na Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya.
tek2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete akizungumza na wageni waalikwa katika halfa ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa NIT, Profesa Blasius Nyichomba.
tek3
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Blasius Nyichomba akifafanua jambo wakati wa halfa ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete.
tek4
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya akifafanua jambo wakati wa halfa ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Blasius Nyichomba.
tek5
Mkuu wa Idara ya Tehama kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Leticia Edward Mihayo akielezea jambo wakati wa halfa ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete na jamboMwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Blasius Nyichomba.
tek6
Mwakilishi Mkazi wa Shirikala la Kimataifa la International Computer Driving Licence (ICDL), Edwin Masanta akizungumza jambo wakati wa halfa ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.
tek7
Mratibu wa Mafunzo ya Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS) Bw. Isaya.J akizungumza jambo wakati wa halfa ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini. Kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Blasius Nyichomba.
tek8
: Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.
tek9
Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.
tek10
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete(kushoto) akimsikiliza Mkufunzi wa Uhandisi wa Ndege Mhandisi Abubakar Noor alipotembelea chumba cha mafunzo ya urubani katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Blasius Nyichomba na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya.
tek11
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete akiwakabidhi vyeti vya kutambulika kuwa wakufunzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System kutoka Idara ya Tehama (CCT) NIT wakati wa hafla ya uzinduzi wa kozi hizo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya.
tek12
tek13
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete akipokea Cheti kutoka kwa Mwakilishi wa ICDL Afrika, Bw. Edwin Msanta (kulia) kwa niaba ya NIT ikiwa ni ithibati ya uanzishwaji wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya.
tek14
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete akikata utepe ikiwa ni ishara wa uzinduzi wa jengo la maabara ya Kopmpyuta kwa ajili ya mafunzo ya Kozi mpya za International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) zitakazokuwa zikifundishwa katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa NIT, Profesa Blasius Nyichomba.
tek15
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete akiangalia Kopmyuta mara baada ya kufungua rasmi jengo la maabara ya Kopmpyuta kwa ajili ya mafunzo ya Kozi mpya za International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) zitakazokuwa zikifundishwa katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa NIT, Profesa Blasius Nyichomba.
tek16
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Tehama kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) mara baada ya kuzindua Kozi mpya za International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) zitakazokuwa zikifundishwa katika Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.
………………………………………………………………………….
Na: Frank Mvungi – MAELEZO
Serikali kupitia Chuo cha Usafirishaji (NIT) imedhamiria kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutekeleza azma ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Ili kufanikisha azma hiyo Serikali imepanga kutumia chuo hicho kuwa kitovu cha kuzalisha
wataalamu watakaozalisha ajira na kuchangia kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete wakati akizindua kozi za International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS).
“Nimefarijika sana kusikia kwamba mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yajulikanayo kama International License (ICDL) yanayotolewa katika nchi zipatazo 100 kote duniani sasa yatakayopatikana  katika Chuo chetu cha Usafirishaji (NIT) kwa gharama nafuu” alisisitiza Madete.
Akifafanua Madete amesema kuwa kwa sasa TEHAMA ikitumika ipasavyo itawanufaisha wananchi kiuchumi na kijamii kupitia Sera Mpya ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2016.
Pia Madete alibainisha kuwa hatua ya kukuza TEHAMA katika Chuo cha Usafirishaji itaongeza ufanisi katika utekelezaji wa juhudi nyingine za Serikali zikiwemo utekelezaji wa mfumo wa anuani za makazi na postikodi unaowezesha utambuzi wa makazi kwa kila mwananchi.
Faida nyingine ni kuiwezesha Serikali kutoa huduma kwa wananchi wake kwa urahisi na ufanisi na pia kusaidia katika ukusanyaji wa kodi.
Mafunzo yatakayotolewa na Chuo cha Usafirishaji ni hatua muhimu kwa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa yanawezesha Taifa kuwa na wataalamu wanaozalisha ajira na ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko kwa sasa.
Kaimu Mkuu wa Chuo hicho  Mhandisi Dkt. Prospar Mgaya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo hicho alisema kuwa chuo hicho kimejipanga kujenga maabara 10 kwa ajili ya mafunzo (TEHAMA).
Naye mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Prof. Blasius Nyichomba alisema kuwa dhamira ya chuo hicho ni kuwa kitovu cha mafanikio ndio maana kimeweza kuwa na kozi zinazotambulika kimataifa.
Aliongeza kuwa kozi zinazotolewa na chuo hicho zinalenga kutatua changamoto katika sekta ya Usafirishaji, Masoko,TEHAMA na nyingine kulingana na mahitaji ya wakati.

No comments :

Post a Comment