SAMATTA AWAPA NENO WACHEZAJI WA BONGO
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania
Taifa Stars Mbwana Samata amewataka wachezaji wa Tanzania kuendelea kuwa
na nidhamu ya mchezo kwa kuwa nchi hii imebalikiwa kuwa na wachezaji
wenye nidhamu ya hali ya juu.
Samata amewataka wachezaji hao kujituma
zaidi pale wanapopata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi
kwani kujituma kwao kutakuwa tija kwa timu ya Taifa kuwa na wachezaji
bora.
Alisema kwamba endapo jambo hilo
litafanywa kwa kila mchezaji atakaepata nafasi ya kwenda kucheza soka la
kulipwa anaamini kila mmoja atafanikiwa zaidi katika soka.
No comments :
Post a Comment