Naibu Waziri Mpina (katikati)
akiwa na ujumbe wake, akisisita jambo wakati wa ukaguzi wa mradi wa
upandaji na utunzaji mikoko katika Delta ya Rufiji kaskazini.
Naibu Waziri Mpina (kaikati) na
Ujumbe wake katika picha wakitembea kukagua mikoko iliyopandwa katika
Delta ya Kaskazini Rufiji.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na ujumbe wake wakiwa
katika Boat, wakielekea katika ukaguzi wa upandaji na utunzaji wa
Mikoko, pamoja na uharibifu wa Mazingira katika Delta ya Rufiji
Kaskazini.
Naibu Waziri Mpina akiwaasa
wasimamizi wa mradi wa upandaji na utunzaji mikoko katika delta ya
kaskazini Rufiji hawapo pichani wamueleze ukweli kuhusu matumizi ya
fedha na hali halisiya mradi kabla ya kwenda kukagua upandaji, utunzaji
wa mikoko na uharibifu wa mazingira.
…………………………………
NA – EVELYN MKOKOI -RUFIJI
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina
amebaini madudu katika matumizi ya sh. milioni 396 za ufadhili wa Mfuko wa
nchi maskini zaidi duniani (LDCF) chini ya mkataba wa dunia mabadiliko ya tabia
amebaini madudu katika matumizi ya sh. milioni 396 za ufadhili wa Mfuko wa
nchi maskini zaidi duniani (LDCF) chini ya mkataba wa dunia mabadiliko ya tabia
nchi katika utekelezaji wa mradi wa upandaji na uendelezaji wa mikoko
katika delta ya kaskazi mto Rufiji.
Katika mradi huo matumizi ya zaidi ya sh. milioni 364 mchanganuo wake
hauridhishi huku vikundi vinavyodaiwa kulipwa fedha hizo vikikana kulipwa
na kusema hawakuwa na mkataba bali walifanya kazi kama vibarua kwa posho ya
sh. 10000 kila wanapomaliza kazi na hawakuwa na mkataba.

Kutokana na hatua hiyo Mpina
amemuagiza Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Makamu wa Rais, Mwatano Maganga
kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anafanya uhakiki wa matumizi ya fedha
hizo za mradi na kuelekeza hatua za kuchukua kwakuwa
vielelezo alivyokabidhiwa na Msimamizi wa mradi kutoka Halmashauri ya
Rufiji Sabastian Gaganijas vina mashaka. “Naagiza ukaguzi ufanyike, lazima kuna ubadhilifu umefanyika katika utekelezaji wa mradi, baada ya ukaguzi makini, tutajua ukweli na kubaini hatua gani zitachukuliwa.” Alisisitiza Mpina.

Hata hivyo, baada ya zoezi zima la kukagua Delta hiyo yenye kilomota zaidi ya
15 Naibu Waziri Mpina, alisema amesikitishwa na jutekelezaji wa mradi huo unaotumia fedha za wafadhili zaidi ya sh.milioni 396 kuwa na madudu na amejionea mwenyewe kuwa, mradi hauna usimamizi na kusema kuwa, kuna
dalili ya fedha hizo kutumika ndivyo sivyo kwakuwa hata hekta 792 kati ya
1000 zilizodaiwa zimepandwa ni udanganyifu wa wazi.

“Huu ni uhuni ambao haukubali kwa serikali hii awamu ya tano tuliposema
hapa kazi tu tulimaanisha kuwa hatuwezi kudanganywa watu wamezoea kuona
Waziri hawezi kuja kwenye mazingira kama haya nimejionea mwenyewe mikoko
iliyopandwa haendani na thamani ya matumizi ya fedha hizo na sehemu kubwa
imevamiwa na kupandwa mpunga badala ya mikoko,”alisema.

Alisema katika mchanganuo aliokabidhi na msimamizo wa mradi fedha hizo
zaidi ya sh.milioni 364 zimedaiwa matumizi yake ni pamoja na kulipa
vikundi 28 vilivyokabidhiwa mradi ambavyo sasa havipo.
zaidi ya sh.milioni 364 zimedaiwa matumizi yake ni pamoja na kulipa
vikundi 28 vilivyokabidhiwa mradi ambavyo sasa havipo.
Alisema cha kushangaza katika fedha hizo kipo kikundi kimelipwa zaidi ya
milioni 30 kwa kupanda hekta 3 huku kingine kikilipwa milioni 3 kwa hekta
hizo hizo.
milioni 30 kwa kupanda hekta 3 huku kingine kikilipwa milioni 3 kwa hekta
hizo hizo.
Baadhi ya wakazi wa rufiji
wakizungumza katika ziara ya Naibu Waziri Mpina, wametoa changamoto zao
katika kukabiliana na uharibifu huo wa Mazingira na kuiomba Serikali
kuongeza usimamizi madhubuti katika mradi huo ili kukubaliana na
uharibifu huo wa hifadhi hiyo ya mikoko,
Awali Imeelezwa na mtaalam wa
Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Cretus Shengena kuwa,
uharibifu huo waMikoko unaweza kusababisha kupotea kwa uoto asili na
baiyonuwai katika eneo hilo kama udhibiti wa dhati usipo chukuliwa kwa
haraka kuinusuru eneo hilo la Delta ya Rufiji kaskazini.
Mradi huo wa hifadhi ya taifa ya
Delta ya Rufiji kaskazini unafadhiliwa na Mfuko wa kundi la nchi maskini
zaidi duniani (LDCF) kupitia Shirika la umoja wa Mataifa ya Mazingira
chini ya usimamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.
No comments :
Post a Comment