Wednesday, March 22, 2017

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA UJENZI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU NYERERE

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr.Leonard Chamriho akitoa taarifa fupi ya wizara kuhusiana na ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea kuona ujenzi wa jengo hilo
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB), Mhandisi Prof. Ninatubu Lema akielezea masuala mbalimbali ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipofanya ziara kwenye jengo hilo linaloendelea kujengwa na linatarajiwa kumalizika Desemba 2017
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi akisoma taarifa ya mradi wa jengo la tatu la abiria (TBIII), kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, ilipofanya ziara kuangalia maendeleo ya ujenzi huo
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Norman Sigalla akiwaeleza jambo wajumbe wa kamati hiyo, wakati wakitembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
Mbunge Charles Kitwanga wa kwanza kushoto akifurahia jambo na wajumbe wenzake wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, leo wakati walipotembelea jengo la tatu la abiria la kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

MAHOJIANO NA DJ D OMMY NDANI YA KILIMANJARO STUDIOS U.S.A

BALOZI SEIF AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA TVH MJINI CHENNAI, INDIA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwasha mshumaha mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Kampuni ya Ujenzi wa Nyumba za Mkopo katika Jimbo la Chennai Nchini India. Kushoto ya Balozi Seif ni Rais wa Jumuiya ya Makampuni ya Nichan Nchini India Bwana Manohar Nichani, Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Dr. Sira Ubwa Mambora, Kayibu Mkuu Wizara ya Kilimo Nd. Juma Ali na Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini India Balozi Mohamed Hij.Kulia ya Balozi Seif ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini India Bibi Haika Msuya na Mwakilishi wa Taasisi ya Kitaifa ya mpango wa kilimo kinachotumia mbolea za Asili India Bwana Satyajit Kittur Mjini
Chennai.

Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akizungumza na Mwakilishi wa Taasisi ya Kitaifa ya mpango wa kilimo kinachotumia mbolea za Asili India Bwana Satyajit Kittur Makao Makuu ya Kampuni ya Ujenzi ya Nchini India Mjini Chennai.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Kimataifa ya Miot Dr. Malika Mohandazaz kwenye Hotelli ya Crowne Plaza Mjini Chennai kabla ya kurejea Mjini New Delhi
Mke wa Makamu wa Pili wa Raios wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akibadilishana mawazo nammoja wa Viongozi Wandamizi wa Hospitali ya Miot Mjini Chennai kabla ya Kuelekea Mjini New Delhi.

Picha na – OMPR – ZNZ.

MKUTANO WA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI WAWAKUTANISHA WADAU JIJINI MWANZA

Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa, akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa mkutano wa mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka, uliofanyika Jijini Mwanza.

                                                                                                         Judith Ferdinand, BMG
 

Maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambyo ni Mwanza, Kigoma, Kagera,Geita, Mara, Shinyanga, Simiyu pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, wamenufaika na elimu kuhusu sheria namba 4 ya mwaka 2010, kwenye sekta ya ujenzi.

Elimu hiyo imetolewa leo katika ufunguzi wa mkutano wa mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka, uliofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa amesema, malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu,ili kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 4 ya mwaka 2010 bila vikwazo pamoja na kujitambulisha kwa wadau,shughuli za bodi,kuelimisha umuhimu wa kuwatumia wataalamu katika shughuli za ujenzi.

Dkt. Mwakyusa amesema, wameona watumie utaratibu wa kuelimisha Maofisa wa Jeshi la Polisi na ofisi ya DPP,ili waelewe sheria hiyo na waweze kutoa msaada wa haraka pale unapohitajika.

Pia amesema,Bodi imesajili wataalamu 1442 lakini wamaotenda kazi ni wacheche kutokana na wengine kuwa walimu vyuoni, hivyo wameona jeshi la Polisi ndio wenye uwezo wa kuwasaidia pale ujenzi unapoanza kama umefuata taratibu za kiserikali kwa kufatilia stika na vibao vinavyobandika kama ilivyo kwa bima na leseni kwa dereva.


Kamishna wa Polisi (Operesheni na Mafunzo), Nsato Marijani akiongea.
 

Kwa upande wake Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani ambaye ndiye mgeni rasmi amesema, jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na Bodi hiyo, katika usimamizi wa sheria pamoja na kuchukua hatua stahiki kwa mtu yoyote atakayeenda kinyume na maelezo ya Sheria namba 4 ya mwaka 2010.

Aidha ameiomba, Bodi hiyo kutoa ushirikiano hasa pale ushahidi unapotakiwa kwa muda muafaka,kwani kila fani ina wataalamu wake.

"Ikumbukwe kila fani inawataalamu wake, hivyo ushirikiano wenu katika kutoa taarifa za kitaalamu utasaidia sana wataalamu wa jeshi la Polisi kuchukua hatua syahiki kwa wakati na wepesi," alisema Marijani.

Naye DPP Mganga amesema, siyo wapelelezi wote wana taaluma ya uhandisi, hivyo kujua chanzo cha jengo kubomoka mpaka wapate ushirikiano kutoka kwa wahandisi.

Kadhalika amesema,mtu yoyote atakayefanya kosa katika ujenzi na kuwepo kwa ushahidi atafikishwa mahakamani

NYOKA NUSURA AZUE KIZAA ZAA KWENYE NDEGE BAADA YA KUTOROKA

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI MAURITIUS

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya watanzania wanasoma na wale wanaoishi nchini Mauritius baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Meridien nje kidogo ya mji wa Port Louis, Machi 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wanaoishi nje ya nchi wazingatie sheria za Taifa husika na kamwe wasijihusishe na biashara haramu ya dawa za kulevya.

“Vita ya dawa za kulevya ni kubwa, hata hivyo Serikali tunaendelea kupambana nayo. Nchi ilikuwa inapoteza vijana ambao walikuwa wamejiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya. Nawaomba msithubutu kuingia huko mtafungwa,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Machi 22, 2017) wakati akizungumza na Umoja wa Watanzania wanaoishi nchini Mauritius katika mkutano alioutisha kwenye hoteli ya Meridien mjini Port Louis.

Amesema katika kudhibiti biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya Serikali iliamua kuunda Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) na inafanya kazi vizuri. “Na tutakamata kila mtu anayejihusisha na biashara hiyo bila kujali cheo, uwezo na mamlaka aliyonayo,”.

Amesema mamlaka hiyo inafanyakazi ya kutafuta wazalishaji, watumiaji na wafanyabiashara, lengo likiwa ni kuokoa vijana ambao wameshindwa kutimiza ndoto zao kutokana na madhara waliyoyapata baada ya kutumia dawa za kulevya.

Katika hatua nyinngine, Waziri Mkuu amewataka Watanzania hao walioko nchini Mauritius kujenga mshikamano wa pamoja na wawe na uzalendo na nchi yao. Pia wawe mabalozi wazuri wa kutangaza vivutio vya Taifa.

Amesema ni vema wakatumia fursa walizonazo katika kutafuta wawekezaji na kuwashawishi waje nchini na kuwekeza kwenye sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda, uvuvi, nishati na utalii.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed amewaomba Watanzania hao wazidishe mshikamano miongoni mwao kwa kuwa umoja wao ndiyo nguzo yao.

“Mko hapa kwa ajili ya kutafuta elimu na wengine mnafanya kazi, shughuli ambazo zitawasaidia kuboresha maendeleo yenu na Taifa kwa ujumla, hivyo nawaomba mzingatie kilichowaleta,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa muda wa Umoja wa Watanzania waishio nchini Mauritius, Bw. Donald Kongwa ambaye ni Ofisa wa benki ya Standard Chaetered nchini Mauritius amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba kipato wanachokipata watakitumia kwa kuwekeza Tanzania kwa lengo la kukuza uchumi wa Taifa.

Aidha, amesema wanaunga mkono na kupongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kujenga uchumi wa viwanda, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, ujenzi wa miundombinu ya kisasa, ununuzi wa ndege pamoja na kuimarisha uwajibikaji na nidhamu kwa watumishi wa umma.

IMETOLEWA NA: 

OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMATANO, MACHI 22, 2017.

RUBANI AKUTWA AKIWA AMELEWA CHAKARI MUDA MCHACHE KABLA YA KURUSHA NDEGE

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU NA KATBU WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) NDUGU GUO JINLONG

SUYA
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akimkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong Ikulu jijini Dar es salaam kwa mazungumzo leo Jumatano Machi 22, 2017
SUYA 1
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akitambulishwa kwa ujumbe aliofuatana nao Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017
SUYA 2
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017
SUYA 3
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongozana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017
SUYA 4
Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mhe Guo Jinlong alipokuwa akisalimia viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Machi 22, 2017

WAZIRI MKUU AHAMASISHA WAWEKEZAJI KUJA NCHINI

TANZANIA NA CHINA ZATILIANA SAINI MKATABA WA MIAKA MITATU WA MASUALA YA UTAMADUNI

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia) wakibadilishana mkataba wa makubaliano utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya nchi hizo wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Serena ijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati), akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei (kulia). Kushoto ni Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Profesa, Elisante Ole Gabariel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto), na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Dong Wei wakiangalia zawadi.

No comments :

Post a Comment