Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Ndg.
Andrew W. Massawe akimpokea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh.
Mwigulu Nchemba(Mb) mara baada ya kuwasili katika ofisi za NIDA makao
makuu.
wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Bunge wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Adad Rajab
(Mb) wakiwasili katika makao makuu ya ofisi za NIDA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mh. Mwigulu Nchemba (MB) akisalimiana na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Bunge Mh. Adad Rajab (Mb) wakati wa ziara ya kamati hiyo
katika ofisi za NIDA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mh. Mwigulu Nchemba akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
Mambo Nje, Ulinzi na Usalama walipowasili NIDA kutembelea na kukagua
maendelea ya mradi wa Vitambulisho vya Taifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama Mh. Adad Rajab (Mb), akiongea
jambo wakati wa kikao na Menejimenti ya NIDA baada ya kupokea taarifa ya
Utekelezaji toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Bw. Andrew W.
Massawe. Kulia ni Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Kanali Mstaafu
Ramadhani Issa Abdallah(Mb).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw.
Andrew W. Massawe, akisoma ripoti ya Utekelezaji Mradi wa Vitambulisho
vya Taifa kwa kamati ya ulinzi na Usalama ya Bunge. Kushoto ni Mh Sophia
H. Mwakagenda(Mb) na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Nchi Mh. Balozi Simba Yahya.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Mh. Mwigulu Nchemba pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Bunge wakisikiliza jambo wakati walipotembelea kituo cha
uchakataji taarifa cha NIDA (NIDA DATA CENTER). Katikati ni Mh. Adad
Rajab(Mb) mwenyekiti wa kamati na kulia ni Mh. Sophia H. Mwakagenda(Mb)
Mjumbe wa kamati
Afisa uzalishaji Vitambulisho
vya Taifa Bw. Jeremiah Kivelege akitoa maelekezo kwa wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama hatua za uzalishaji
Vitambulisho vya Taifa walipotembelea kituo kikuu cha Uhifadhi na
uchakataji wa Taarifa (Data centre)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA
Bw. Andrew W. Massawe akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge Mambo Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu ubora wa
Kitambulisho.
……………..
Kamati ya Kudumu ya Bunge
Mambo Nje, Ulinzi na Usalama leo imefanya ziara ya kukagua mradi wa
Vitambulisho vya Taifa; ambapo mbali na kupokea taarifa ya utekelezaji
pia
walitembelea na kukagua kituo kikuu cha Kuhifadhi, kuchakata na
kuzalisha Vitambulisho vya Taifa -Data Centre.
Akizungumza wakati wa
kukaribisha Kamati hiyo; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu
Lameck Nchemba (Mb) amesema mpaka sasa NIDA imefanikiwa kutekeleza
majukumu yake kwa kiwango kikubwa pamoja na changamoto kubwa ya fedha
iliyopo.
Akizungumza kwa niaba ya
Kamati hiyo; Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Adad Rajab (Mb) amepongeza
jitihada kubwa zinazofanywa na NIDA na kwamba Kamati imeridhishwa na
kazi kubwa na nzuri inayofanywa na NIDA na kwamba Kamati yake itaendelea
kuishauri Serikali kuongeza bajeti ya fedha kwa NIDA ili kuwezesha
kukamilisha zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa, kwani manufaa ya
kuwa na mradi huu kwa Taifa ni makubwa katika Nyanja zote.
Wakitoa maoni yao wajumbe wa
Kamati hiyo wameitaka Wizara kuiwezesha NIDA na kuharakisha matumizi ya
Vitambulisho vya Taifa kielektroniki kwani tayari idadi kubwa ya
wananchi wameshatambuliwa na taarifa zao kuingizwa kwenye mfumo.
“Kutokana na manufaa makubwa
ya mradi huu kwa Taifa, Serikali ihakikishe inatumia kila mbinu
kuhakikisha matumizi yaliyokusudiwa ya kuwa na Vitambulisho vya Taifa”
Akisoma taarifa yake kwa
Kamati hiyo; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Andrew W. Massawe
ameieleza Kamati hiyo mpaka sasa NIDA imekamilisha Usajili wa Watumishi
wa Umma nchi nzima ambapo watumishi 500,605 wamesajiliwa, NIDA imeanza
kuwasajili wageni wanaoishi kihalali nchini, kufungua ofisi katika
Wilaya zote nchini pamoja na kuanza zoezi la kuwasajiliwa wananchi
katika mikoa mbalimbali nchini akiitaja baadhi; Lindi, Iringa, Geita,
Singida, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Manyara n.k.
No comments :
Post a Comment