Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa
tatu kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za
Serikali (PAC), kabla ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Bunju B
jijini Dar es Salaam jana zinazojengwa na wakala huo. Wa pili kulia ni
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
Baadhi ya maofisa wa TBA wakiwa kwenye mkutano na
wajumbe wa kamati hiyo.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa
pili kushoto), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za
Serikali (PAC), walipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba Bunju B jijini
Dar es Salaam jana. Wa nne kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,
Josephat Asunga.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo.
Baadhi ya nyumba zinazojengwa katika mradi wa Bunju B
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga, akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo.
Baadhi ya nyumba zinazojengwa kwenye mradi wa Bunju B
Mwonekano wa nyumba hizo.
Na Dotto Mwaibale
WATUMISHI
wa Umma wametakiwa kuchangamkia nyumba zinazojengwa na Serikali kupitia
Wakala wa Nyumba Tanzania (TBA), ili kupata makazi bora baada ya
kustaafu.
Wito huo
umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC), Josephat Asunga wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea
miradi ya ujenzi wa nyumba inayofanywa na TBA jijini Dar es Salaam
jana.
“Nawaomba
watumishi wa umma kuzichangamkia nyumba hizi ambazo kwa wao wanafursa
ya kukopeshwa na kulipa deni polepole” alisema Asunga.
Alisema nyumba hizo zimejengwa na kuwekewa miundombinu mizuri hivyo kuwa ni sehemu bora ya kuishi.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Nyumba Tanzania (TBA), Mhandisi Elius Mwakalinga
alisema nyumba zinazojengwa na TBA bei yake ni ndogo ukilinganisha na
zile zinazojengwa na watu wengine.
“Hapa
kwetu bei ya nyumba inaanzia sh.milioni 35 hadi milioni 200 wakati
maeneo mengine ni kuanzia sh.milioni 600” alisema Mwakalinga.
Alisema
ujenzi wa nyumba hizo unakwenda sanjari na miundombinu yake na mahitaji
mengine kama soko, bustani na maegesho ya magari.
Alisema
katika awamu ya tatu ya mradi TBA walipata mkopo wa sh.Bilioni 25 ambapo
hadi Februari 2017 walipata mkopo wa sh.Bilioni 19.5 kwa ajili ya
ujenzi wa nyumba za kuwauzia watumishi wa umma.
Alisema
katika awamu ya pili ya mradi huo jumla ya nyumba 160 za aina tofauti
zinaendelea kujengwa za zipo katika hatua mbalimbali, ambapo nyumba 64
zipo kwenye hatua za mwisho tayari kwa kuuzwa na nyumba 96 bado zipo
kwenye hatua ya msingi na zilitarajiwa kujengwa kwa kutumia mfumo wa
“Lunnel Forwork System”
Akizungumzia
changamoto katika mradi huo alisema watu kujenga nyumba katika baadhi
ya viwanja ndani ya eneo la mradi hivyo kupunguza idadi ya nyumba
zilizokusudiwa kujengwa katika hatua za awali za awamu ya tatu ya mradi.
Alitaja
changamoto nyingine kuwa ni kupatikana kwa malighafi mbalimbali za
ujenzi hasa mawe, nondo hivyo kupunguza kasi ya ujenzi, upungufu wa
fedha za utekelezaji wa mradi, kupanda kwa gharama za ujenzi kutokana na
kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi.
Alisema ili kupunguza gharama za kununua vifaa vya ujenzi wakala amekuwa akienda kuvinunua moja kwa moja kiwandani.
No comments :
Post a Comment