Wednesday, March 22, 2017

DIWANI KIJICHI AKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHAKE


ASUK
Habari kuhusu kifo cha diwani wa kata ya Kijichi Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Tausi Milanzi zimekuwa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii jambo lililopelekea Mtembezi Media Group kutafuta ukweli wa jambo hilo.
Mtembezi ilimtafuta diwani huyo kwa njia ya simu ya kiganjani na kuzungumza nae ambapo amekanusha uwepo wa taarifa hizo na kueleza kuwa yeye ni mzima wa afya na anaendelea na shughuli zake kama kawaida na kuwataka wananchi wake waendelee kumuunga mkono na kupuuza uvumi huo.
Pia amehaidi kuwafikisha katika vyombo vya sheria wote wanaosambaza taarifa hizo kwa ni matumizi mabaya ya mtandao na ni kinyume na sheria ya mitandao ya hapa nchini.

No comments :

Post a Comment