Tuesday, March 28, 2017

BILA SAMATTA STARS YAILAZA BURUNDI YA MAVUGO VV

VV
Na.Alex Mathias
Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshindi mchezo wa pili Mfululizo wa Mechi za Kirafiki baada ya kuwatandika majirani zao Burundi magoli 2-1 mchezo uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Wakicheza bila Nahodha wao Mbwana Samatta aliyeondoka leo na kurejea Ubelgiji kujiunga
na timu yake ya KRC Genk,alikuwa winga hatari kwa sasa Simon Msuva aliifungia Stars dakika ya 20 shuti la moja kwa moja akipokea pasi ya Ibrahim Ajibu.
Hadi mapumziko Stars walikuwa mbele kwa goli moja hilo huku Vijana wa Mayanga wakicheza Mpira wa kuonana na wachezaji kuweza kutulia japo kosa kosa zilikuwa nyingi kupitia kwa Msuva.
Kipindi cha pili, mshambuliaji Laudit Mavugo akatumia makosa ya mchezaji mwenzake wa Simba, beki Abdi Banda kuifungia bao la kusawazisha Burundi.
Mavugo aliutokea mpira uliompita Banda na kwenda kumtungua kipa wa Yanga, Deo Munishi ‘Dida’ dakika ya 53.
Pamoja na Burundi kusaka bao la pili kwa juhudi, lakini walijikuta wakifungwa wao na kulala 2-1.
Chipukizi, Mbaraka Yussuf Abeid ameanza vyema soka ya kimataifa baada ya kutokea benchi na kuifungia bao la ushindi Tanzania ikiilaza 2-1 Burundi katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezaji huyo wa Kagera Sugar ya Bukoba, alifunga bao hilo dakika ya 77 baada ya kupokea pasi ya Simon Msuva mbele kidogo ya mstari unaogawa Uwanja na kujivuta hadi ndani ya boksi kabla ya kufumua shuti lililogonga mwamba na kurudi, akauwahi na kufunga bao zuri.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Salim Mbonde, Himid Mao, Muzamil Yassin/Jonas Mkude, Salum Abubakr ‘Sure Boy’/Said Ndemla, Ibrahim Hajib/Shiza Kichuya, Farid Mussa/Mbaraka Yussuf na Simon Msuva.
Burundi; Jonathan Nahimana, Gael Duhayindavya, Rashid Harerimana, Omary Moussa, David Nshirimimana/Eric Ndoyirobija, Youssouf Ndayishimiye, Tresor Ndikumana, Jean Ndarusanze/Franck Barirengako, Laudit Mavugo, Kiza Fataki/Moustapha Selemani na Djuma Nzeyimana/Sudi Ntirwaza.

No comments :

Post a Comment