Sunday, March 26, 2017

AGPAHI YAADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA KIFUA KIKUU – MERERANI, MKOA WA MANYARA




 Bi. Alio Hussein akiwaonesha kwenye picha namna ambavyo vijidudu vya Kifua Kikuu vinaweza kusambaa kama mgonjwa atakohoa bila kuziba mdomo, wakati wa semina ya elimu ya namna ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza yaliyoendeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa wachimbaji wadogowadogo wa madini huko Mererani mkoani Manyara.
NA MWANDISHI WETU Shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojishughulisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limeungana na wadau wote duniani katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani, 24 March 2017.

Maadhimisho hayo yalifanyika katika mji mdogo wa Mererani, wilaya ya Simanjiro katika Mkoa wa Manyara, eneo ambalo Shirika la AGPAHI linatekeleza mradi wa kutoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI sehemu za migodini kwa hisani ya shirika la ADPP la Msumbiji.
Katika maadhimisho hayo, shirika la AGPAHI kwa kushirikiana na timu ya afya ya wilaya walifanya zoezi la kutoa huduma mbalimbali kwa jamiii inayozonguka mji mdogo wa Marerani kuanzia tarehe 23 – 25 Machi, 2017.
Huduma zilizotolewa ni uchunguzi wa kifua kikuu, kupima Virusi vya Ukimwi na kutoa elimu kwa umma kuhusu kifua kikuu na VVU/UKIMWI.
Zoezi hilo lilisimamiwa na afisa mradi wa kifua kikuu na UKIMWI, kutoka AGPAHI, mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya ya Simanjiro, wataalamu wa maabara, watoa huduma wa Afya kutoka kituo cha Afya Mererani na wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani ni; “TUUNGANE PAMOJA KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU”.

Shirika la AGPAHI linafanya kazi katika mikoa sita ambayo ni Mwanza, Geita, Mara, Tanga Shinyanga na Simiyu. Huduma zitolewazo na shirika la AGPAHI ni kusaidia serikali kupitia vituo vya kutolea huduma za afya katika:
   1.Kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu
      wanaoishi na virusi vya UKIMWI;
   2.Kutoa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya
      UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto;

   3.Kutoa huduma ya uchunguzi wa dalili za awali na
      huduma za awali za saratani ya mlango wa kizazi
      na
    4.Kutoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI
     sehemu za migodini.
Vilevile, shirika linafanya kazi katika mji mdogo wa mererani katika kutekeleza mradi wa kifua kikuu sehemu za migodini.

Afisa mradi wa Kifua kikuu na UKIMWI kutoka AGPAHI, Bi Alio Hussein akiwaelimisha na kugawa vipeperushi kwa wakazi wa Mererani kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI.


Mhudumu wa afya ngazi ya jamii akiwaelezea wakazi wa Mererani dalili za Kifua Kikuu na namna ya kuweza kujikinga na maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.


Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wakichukua maelezo ya baadhi wakazi wa Mererani waliokua tayari kuchunguzwa kama wana maambukizi ya vijidudu vya Kifua Kikuu.


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Kajolii Maasai akitoa burudani na kuendelea kuwahimiza wakazi wa Mererani kuja kupata Elimu kuhusu Kifua Kikuu.


Elimu kwa wachimbaji wa madini ya Tanzanite kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI ikiendelea.


Wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika Kitalu D, wakiwa wamekusanyika kwa wingi wakielimishwa kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI.


Bi. Alio Hussein akiwaonesha kwenye picha namna ambavyo vijidudu vya Kifua Kikuu vinaweza kusambaa kama mgonjwa atakohoa bila kuziba mdomo.


Wachimbaji wakielimishwa kuhusu aina za Kifua
Kikuu kwa njia ya bango.




Maswali mbalimbali yakiulizwa kwa wachimbaji juu ya kifua kikuu na UKIMWI.


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Kajolii Maasai akitoa burudani kwa wachimbaji wa Kitalu D waliokusanyika kwa wingi kuja kupata Elimu kuhusu Kifua Kikuu.


Mchimbaji wa madini ya Tanzanite akijibu swali lililoulizwa ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu na uhamasishaji kuhusu Kifua kikuu na Ukimwi.


Wa kwanza kushoto ni Kajolii Maasai msanii wa muziki wa kizazi kipya, wa pili kushoto ni mchimbaji wa madini ya Tanzanite ambaye alijishindia Tishirt baada ya kujibu vizuri swali kuhusu Kifua kikuu na watatu kutoka kushoto ni Afisa mradi wa Kifua kikuu na UKIMWI, Bi Alio Hussein, na mwisho ni Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma Wilaya ya Simanjairo, Bi Selestina Rosai.

(Na Joshua Fanuel wa Kilimanjaro Official blog).


Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, (PIC) wakitembelea mradi wa uwekezaji nyumba za kisasa za kupangisha za Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa cha Arusha, (AICC), ambapo mradi huu umekamilika na tayari nyumba hizo zimeisha pata wapangaji.(PICHA NA AICC)



NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeushauri uongozi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kuelekeza nguvu ya uwekezji katika mji wa
Dodoma ili kuziba kukidhi ongezeko la huduma za kumbi za kufanyia muikutano linalosababishwa na serikali kuhamia katika mji huo.
Akizungumza katika kikao cha majumuisho baada ya Kamati ya PIC kutembelea AICC mwishoni mwa wiki na kukagua miradi miwili, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Albert Obama ameshauri AICC kuupa kipaumbele mkoa wa Dodoma katika mkakati wa kujenga kituo kingine cha kisasa cha Mikutano.
“Tunahitaji kuiona taasisi hii ikipanuka na kujenga vituo vingine vya mikutano huko mikoani na moja ya mikoa ambayo tungependa muipe kipaumbele ni Dodoma maana huko ndio serikali inahamia na mahitaji ya huduma ya kumbi za mikutano yanakwenda kuongezeka”, alisisitiza Obama.
Nae Mjumbe wa Kamati hiyo, Amina Mollel alieleza kufurahishwa na juhudi za uongozi wa AICC kumilisha ujenzi wa mradi wa nyumba za kisasa (apartment) 48 ambapo azote zina wapangaji na kuwa sehemu muhimu ya kuongeza mapato ya shirika.
Aidha ameushauri uongozi wa AICC kuzingati uwekaji wa miundombinu ya walemavu katika miradi mingine inayotekelezwa ukiwemo mradi wa ujenzi wa ukumbi wa kisasa kwa ajili ya maonesho ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Mei mwaka huu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Elishilia Kaaya aliieleza Kamati ya PIC kuwa Kituo kina mipango ya baadae ya kujenga Kituo kingine cha Kisasa cha Mikutano kitakachojulikana kama Mount Kilimanjaro International Convention Centre (MKICC) ili kukabiliana na ushindani wa biashara ya mikutano kutoka nchi za jirani kama Rwanda ambayo tayari ina Kituo cha kisasa cha Kigali na Kenya ambayo tayari inatarajia kujenga Kituo cha kisasa cha Mikutano huko Mombasa.
Kaaya ameeleza kuwa AICC imefanikiwa kununua ekari 23 katika mji wa Mtwara na pia inatafuta ardhi katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Iringa kwa ajili ya kujenga Vituo vingine vya Mikutano. Aidha alieleza Kamati kuwa mbali na kujenga Vituo vya Mikutano, AICC inatarajia kujenga miundombinu kwa ajili ya Wanajuiya ya Kidiplomasia eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetenga eneo kubwa kwa ajili ya taasisi mbalimbali za kimataifa kujenga ofisi.
Mbali na biashara ya mikutano, AICC inajishughulisha pia na upangishaji wa ofisi na nyumba na pia inatoa huduma za afya kupitia hospitali yake. Pia AICC inamiliki Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kilichopo Dar es Salaam.

No comments :

Post a Comment