Sunday, February 12, 2017

YANGA YAUWASHA MOTO LIGI YA MABINGWA AFRIKA,YAISAMBARATISHA NGAYA FC YA COMORO

  juma-mwambusi-na-wachezaji-yanga_1l9wiebjm5r4l1hffdqpwv58e2
Na.Alex Mathias
Mabingwa Watetezi wa Comoro timu ya Ngaya FC imeanza vibaya katika Michuano ya awali ya Kombe la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kukubali kichapo cha Paka Mwizi toka kwa Mabingwa wa kihistoria nchini Tanzania Yanga cha jumla ya Magoli 5-1 na kujiweka katika nafasi finyu ya kusonga mbele.
Mchezo ulianza kwa kasi huku wachezaji wa Ngaya wakiwa na maumbo makubwa na Warefu
waliwapa shida vijana wa Kocha wa Yanga Lwandamina huku washambuliaji wa Yanga wakikosa nafasi nyingi za wazi na kama wangekuwa makini wangeondoka na magoli mengi.
Dakika ya 43 kiungo mkabaji toka Zambia Justine Zullu alifunga bao la kwanza baada ya kupokea pasi toka kwa Obrey Chirwa na Simon Msuva alifunga la pili dakika ya 45 kwa shuti la Mita 18 ambalo lilimshinda Mlinda Mlango wa Ngaya Said Komandoo hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa magoli mawili.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo wanajangwani waliweza kutumia nafasi ambazo waliweza kuzipata Obrey Chirwa alifunga la tatu dakika ya 59 baada ya Kamusoko kupigia pande la pasi na dakika ya 65 Mshambuliaji mwenye rekodi ya Tuzo Tanzania Amis Tambwe alifunga la nne akipokea krosi toka kwa beki Juma Abdul.
Akitokea benchi Said Khalfan aliifungia Ngaya bao la kufutia machozi baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Yanga dakika ya 66 hata hivyo furaha yao haikuweza kudumu kwani dakika ya 73 Juma Mahadhi alipigilia msumari wa tano kwa pasi safi toka kwa Thabani Kamusoko.
Hadi mwamuzi anamaliza Mpira Yanga wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 5-1 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele hatua inayofuata na timu hizo zinatarajia kurudiana Februari 18 jijini Dar es salaam huku Ngaya wanatakiwa kushinda jumla ya magoli 6-0 ili waweze kusonga mbele na endapo Yanga watasonga mbele watakutana na APR ya Rwanda au Zanaco ya Zambia ambazo jana ziliweza kutoka sare ya bila kufungana na Yanga wanatarajia kurudi siku ya Jumanne na kujiandaa na mchezo wa marudiano

No comments :

Post a Comment