Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi
wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) David Kanyatta akiwasilisha mada kwa
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu madhara
ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi kunavyoathiri sekta ya utalii
katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma .
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii, Yussuf Hussein, akichangia hoja mara baada
ya mada kuweza kuwasilishwa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na
Utalii kuhusu utalii wa baharini ambao umekuwa haupewi kipaumbele
katika kutangazwa pamoja na kuendelezwa katika semina hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii, Marwa Chacha, (katikati) akichangia hoja
mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na wataalamu kutoka Wizara ya
Maliasili na Utalii kuhusu wanyamapori waharibifu wa mazao kama vile
tembo wanavyoathiri maisha ya wapiga kura wake kwenye vijiji
vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika semina iliyofanyika
jana mjini Dodoma. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo .
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii, Atashasta Nditiye, (katikati) Waziri wa
Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ( kushoto) pamoja na Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani ( wa kwanza kulia)
wakifuatilia kwa makini michango ya wajumbe wa kamati hiyo wakati
walipokuwa wkichangia hoja kuhusu mada mbalimbali zilizotolewa na
wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu madhara ya
kulishia mifugo ndani ya hifadhi, tatizo la ujangili wa tembo na faru
pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu wa mazao kama vile
tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini, iliyofanyika jana
mjini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii, Devota Minja, MB ( wa kwanza kulia) pamoja
na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia kwa makini mada
mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa Wizara hiyo
kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi, tatizo la ujangili
wa tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu
wa mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini
katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Kwa upande wa kushoto ni
viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) pamoja na na
viongozi wa taasisi katika semina ya kamati ya Bunge Ardhi,
Maliasili na Utalii iliyofanyika jana mjini Dodoma .
No comments :
Post a Comment