Wednesday, February 15, 2017

Watumishi Muhimbili wakumbushwa kufanya kazi kwa Uadilifu

NE1
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Agnes Mtawa  akitoa neno katika hafla fupi ya kumuaga Muhudumu wa afya  Mama Eda Kapange  iliyofanyika katika Hosppitali ya Taifa Muhimbili.
NE2
Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Idara ya watoto wakishangilia huku wakiinua maua juu kama ishara ya upendo.
NE3
Kushoto ni Mama Eda Kapange akikata keki katika hafla hiyo ya kumuaga, keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga
NE4
Baadhi ya viongozi wakimtakia heri na  afya njema mama Eda Kapange katika maisha yake  baada ya  kulitumikia taifa.
NE5
Baadhi ya wauguzi na Madaktari wa Idara ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.
……………………………………………………………………………..
Dar es salaam
Watumishi wa afya  wamekumbushwa kufanya kazi kwa bidii na  kuzingatia maadili ya taaluma ya kazi ili kuendelea kutoa huduma bora  .
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili  Agnes Mtawa  alipokua akizungumza katika hafla fupi ya kumuaga Muhudumu wa afya  Mama Eda Kapange aliyekua akihudumu katika katika Idara ya watoto.
Amesisitiza kuwa suala la kuzingatia maadili ya taaluma hiyo ni muhimu kwani mgonjwa anahitaji upendo na kupewa maneno yenye matumaini na kwamba hiyo pekee ni tiba .
Pia Mkurugenzi Mtawa  amemuelezea  Mama   Eda Kapange kuwa ni mtumishi hodari na mchapakazi  hivyo  amewataka watumishi wengine kuiga mfano wake kwa vitendo.

No comments :

Post a Comment