Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisikiliza
maoni kutoka kwa Bw. Mohammed Ally mkazi wa Nakapanya, Wilayani
Tunduru, Mkoani Ruvuma kuhusu furaha yao juu ya kukamilika kwa ujenzi wa
Barabara ya Nakapanya-Tunduru KM 66.5.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akionesha
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), picha ya barabara ya
Nakapanya-Tunduru KM 66.5 iliyokamilika kwa kiwango cha lami wakati
alipokuwa akikagua barabara hiyo, mkoani Ruvuma. Kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Tunduru Bw. Juma Homera.
Muonekano wa barabara ya Nakapanya-Tunduru KM 66.5 iliyokamilika kwa kiwango cha lami, mkoani Ruvuma.
Meneja
wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Ruvuma Eng. Lazeck
Alinanuswe (mwenye koti la kaki), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto kwa Meneja), ujenzi wa
kingo za Daraja la Lumesule lililopo mpakani mwa mkoa wa Ruvuma na
Mtwara wakati alipokagua daraja hilo.
Mbunge
wa Jimbo la Nanyumbu Mhe. Dua Nkurua (kushoto), akisisitiza jambo kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
(kulia), mara baada ya kuzungumza na uongozi wa wilaya hiyo, mkoani
Mtwara.
Mkuu
wa Wilaya ya Tunduru Bw. Juma Homera (mwenye koti la kaki), akimuonyesha
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
(kushoto kwa Mkuu wa Wilaya), moja ya ofisi katika jengo jipya la Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya huyo, alipoikagua Wilayani humo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiongea na
uongozi wa Wilaya ya Tunduru, mara baada ya kukagua miradi iliyo chini
ya Wizara hiyo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifurahi
jambo na wafanyakazi wa kampuni ya Korosho, Wilayani Tunduru mara baada
ya kutembelea na kuangalia uzalishaji wa korosho katika kiwanda hicho.
………………………….
Wananchi
wa Nakapanya, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wameridhishwa na kasi ya
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Nakapanya-Tunduru yenye
urefu wa KM 66.5 ambayo imekamilika kwa asilimia Tisini na tisa na
sasa mkandarasi yuko kwenye hatua za kumaliza uwekaji wa alama za
barabarani.
Wakieleza
furaha yao kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa mara baada ya kukagua barabara hiyo, wananchi hao wamesema
kuwa uwepo wa barabara hiyo umechochea maendeleo makubwa katika mkoa huo
na mikoa ya jirani.
“Tunaishukuru
sana Serikali kwani imesikia kilio chetu cha miaka mingi cha kuomba
kujengewa barabara ya lami katika wilaya yetu, sasa tunafurahia matunda
ya ujenzi huu”, amesema Bw. Mohammed Ally.
Kwa
upande wake, Waziri Prof. Mbarawa amewataka viongozi wa Wilaya hiyo na
kamati za ulinzi na usalama kuhakikisha wanawasimamia wananchi katika
kuitunza na kuilinda miundombinu ya barabara hiyo ili iweze kudumu na
kuweza kutumika kwa vizazi vijavyo.
Ameongeza
kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kumeufungua mkoa wa Ruvuma na wilaya
zake pamoja na mikoa jirani ya Mtwara na nchi ya Msumbiji, hivyo
kuchochea fursa za kibiashara kwa kiasi kikubwa.
Kuhusu
huduma za mawasiliano mkoani humo, Waziri Mbarawa amesema kuwa Wizara
yake itahakikisha inapeleka mawasiliano haraka iwezekanavyo katika
maeneo yenye changamoto hususan vijijini.
Naye,
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Juma Homera amemhakikishia Waziri huyo
kuwa atashirikiana kwa ukaribu na viongozi wenzake katika kutekeleza
maagizo yote aliyowapa ikiwemo la ulinzi wa miundombinu ya barabara
hiyo.
Meneja
wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Ruvuma amemuhakikishia
Waziri Prof. MBARAWA kuwa Wakala utatatua changamoto zote
zilizojitokeza wakati wa ujenzi wa barabara ikiwemo fidia kwa wananchi
waliovunjiwa nyumba zao kupisha barabara hiyo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments :
Post a Comment