Mfanyakazi wa Kampuni ya mtandao
wa simu ya Zantel Kitengo cha Uhasibu Bw. Ally Abdallah akichangia damu
kwa hiari wakati wa zoezi la uchangiaji damu salama lililowahusisha
wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kukabiliana na wingi wa
watu wengi wenye uhitaji wa huduma hiyo kila mwaka. Zoezi hilo
lilifanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini
Dar es salaam. (Kushoto) ni Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa damu
Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Cecilia Meena.
Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa
wa damu salama-Kanda ya Mashariki Bi. Cecilia Meena (Kulia) akimaliza
kumtoa damu mfanyakazi wa kampuni ya mtandao wa simu ya Zantel, Abdallah
Ridhwa Mzumbasha wakati wa zoezi la uchangiaji damu kwa hiari ili
kuokoa maisha ya watanzania wengine lililofanyika mwishoni mwa juma
katika makao makuu ya Zantel jijini Dar es salaam.
Mfanyakazi wa Kampuni ya mtandao
wa simu ya Zantel Kitengo cha Ugavi Bi. Mainda Madiwa Chanika akichangia
damu kwa hiari wakati wa zoezi la uchangiaji damu salama
lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kukabiliana
na wingi wa watu wengi wenye uhitaji wa huduma hiyo kila mwaka. Zoezi
hilo lilifanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo
jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa
damu Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Cecilia Meena.
Mfanyakazi wa Kampuni ya mtandao
wa simu ya Zantel Kitengo cha Ugavi Bi. Mainda Madiwa akiweka sahihi
kwenye fomu kabla ya kuingia katika zoezi la hiari la uchangiaji wa damu
salama ili kuokoa maisha ya watanzania wengine lililofanyika mwishoni
mwa juma katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam.
(Kushoto) ni Afisa Uhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa damu
Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Fatuma Mjungu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mauzo ya
jumla wa Kampuni ya Zantel, Deo Ngonyani akishiriki katika zoezi la
uchangiaji damu salama lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa
ni njia mojawapo ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa
huduma hiyo. Zoezi hilo lililifanyika mwishoni mwa juma katika makao
makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam. (Kulia) ni Mwakilishi kutoka
Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Cecilia Meena.
……………………………
Kampuni ya mtandao wa simu Zantel
imeendesha zoezi la kuchangia damu salama ambapo baadhi ya wafanyakazi
wake wamejitolea kufanya zoezi hilo katika kukabiliana na wingi wa
watu
wengi wenye uhitaji wa huduma hiyo kila mwaka.
Zoezi la uchangiaji damu ni moja
ya sehemu muhimu kwa kampuni hiyo katika kuhimarisha uhusiano wake na
jamii kupitia kitengo chake cha uhusiano wa Jamii (CSR). Zoezi hili ni
sehemu ya mwendelezo wa moja ya kampeni ya Kampuni hiyo yenye kaulimbiu ‘Onyesha Upendo na Uwapendao’.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo
la kuchangia damu lililofanyika kwenye makao makuu ya ofisi za Zantel
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma, kwa niaba ya Mkuu wa kitengo cha
Rasilimali watu Zantel, Bw. Frank Jackson alisema kwamba juhudi hizo
zilianzishwa ili kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wagonjwa
wengi wenye uhitaji wa kuongezewa damu hapa nchini huku lengo pia likiwa
ni kuokoa maisha ya wananchi kadri inavyowezekana hususani wakina mama
pamoja na watoto walio chini ya miaka mitano.
“Tunayofuraha isiyo kifani kwa
kukamilisha shughuli hii leo, ambayo kimsingi inaonyesha uhusiano na
wajibu wetu kwa jamii lengo letu likiwa ni kuhimarisha afya za
Watanzania wenzetu,” alisema Bw. Jackson.
Aliongeza kuwa, katika nchi zenye
watu wengi wenye kipato cha chini watoto walio chini ya umri wa miaka
mitano wanahitaji siyo chini ya asilimia 65 ya damu yote inayochangiwa
kila mwaka ili kuokoa maisha yao.
“Sisi kama kampuni tumeona ni
wajibu wetu kushiriki katika zoezi hili la uchangiaji damu ili kuendelea
kuokoa maisha ya wananchi,” alisema.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka
Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki, Bi. Fatuma Mjungu
alisema, “Tumefurahi sana kuungana na baadhi ya wafanyakazi wa Zantel
leo katika kufanikisha zoezi hili ambalo linahitaji uhamasishaji mkubwa.
Tumefurahishwa zaidi na mchango mkubwa ulioonyeshwa na timu ya Zantel
ambayo imethibitisha wazi kwa jinsi walivyokuwa tayari kujitolea katika
kusaidia Watanzania”.
Aliongeza kuwa mahitaji ya damu
nchini bado ni makubwa na bado wanahitaji ushirikiano kutoka kwa watu
mbalimbali ili kuweza kufikia lengo la kukusanya lita 300,000
zinazohitajika kila mwaka ili kuwahudumia watu wenye mahitaji ya huduma
hiyo.
No comments :
Post a Comment