Na Riziki Manfred Bonzuma, Mbinga
Wadau
wa elimu na viongozi halmashauri ya Mbinga vijijini wamekutana kufanya
tathimini ya elimu ikiwemo kushuka kwa ufaulu kwa wa elimu ya msingi
miaka ya hivi karibuni.
Wakizungumza
katika kikao hicho ,baadhi ya wadau wa elimu wamezitaja changamoto
zinazopelekea kushuka kwa elimu kuwa ni pamoja kutoboreshwa kwa masirahi
ya walimu, upungufu wa walimu, ushiriki hafifu wa wazazi hususani
kufuatilia maendeleo ya watoto wao na kuchangia shughuli za elimu.
Pia
wadau wameainisha changamoto zingine kuwa ni pamoja na kuto wahamisha
walimu wakuu walio shushwa vyeo pamoja na kuongeza uwiano wa vitabu hasa
vya kiada katika shule za halmashauri hiyo.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini
Gombo Samandito Gombo amesema halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha
inaongeza ufaulu kimkoa na kitatifa hasa elimu ya msingi ambayo
imeonekana kulegalega huku akiwataka walimu kuto fanya uzembe katika
kufundisha ikiwemo utotoni.
“sitakuwa
na msamaha kwa walimu wanao acha kazi wanaenda kupiga boda boda ukiona
nimekubaini nitakufukuza hata usiangaike kuniomba msamaha pia wapo
walimu wanao kopa mpaka wanapiriliza muda wa kufundisha wanakimbia
madeni waache mara moja” alisema Samandito .
Awali
katika maada za utangulizi mkuu wa Polisi wilaya ya Mbinga OCD Maganga
amekemea baadhi ya wazazi kuwahusisha wanafunzi katika biashara ya dawa
za kulevya na kuwataka viongozi ngazi ya vijijini na kata kutoa taarifa
za wahusika wa biashara hiyo pamoja na wale wanao wapa mimba wanafunzi.
Katika
hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Mbinga Consimas Nshenyi amendelea
kukazia maagizo yaliyo tolewa wa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Binilith
Mahenge wakati wa ziara yake wilaya Mbinga mapema mwaka huu juu ya
uharibifu wa mazingira ikiwemo kufanya shughuli za kibinaadamu ndani ya
mita sitini kutoka vyanzo vya maji pamoja na kuhakisha Benki tofauti
zinatukamika katika kujenga majengo sio kukaa katika matanuru .
Matokeo
ya darasa la saba mwaka 2016 yanaonyesha kushuka kwa elimu katika
halmashauri hiyo ya wilaya ya Mbinga baada ya kushika nafasi ya 8 katika
mkoa wa Ruvuma kati ya Halamashauri 8 za mkoa huo.

No comments :
Post a Comment