Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wadau
wa sekta ya filamu (hawapo pichani) wakati wa kikao cha wadau
kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu
Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura na
Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Millao
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo
wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu
leo Jijini Dar es Salaam.
Mtayarishaji na msambazaji wa
filamu nchini Bibi. Rose Urio akichangia mada wakati wa kikao cha wadau
wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa
la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitolea ufafanuzi maoni
yaliyotolewa wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia
sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango
kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Petro Ryatuu
akizungumza na wadau wa sekta ya filamu (hawapo pichani) wakati wa kikao
cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta ya
filamu wakisikiliza hoja zilizokua zikiendelea kutolewa wakati wa kikao
cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wanne kulia) katika picha ya
pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya filamu walioshiriki katika kikao
cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Watatu
kulia ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Annastazia Wambura, watano kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof.
Elisante Ole Gabriel na wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Bibi. Nuru Millao
Picha na: Genofeva Matemu WHUSM
No comments :
Post a Comment