Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa kilele cha
Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini
Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa
Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na
Filamu,Mila na desturi zake”.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla akizungumza wakati wa kilele
cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana
jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya
“Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza
Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran
nchini Tanzania Mossa Farharng (wa pili kutoka kushoto) akifuatilia
hotuba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses
Nnauye (hayupo pichani) wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz
iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam
jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax
Mabulla, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran Ali Bagheri na
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akicheza Bao na Mwenyekiti wa
Shirikisho la Michezo ya Jadi Tanzania Bw. Mohamed Kazingumbe (kulia)
wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na
Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli
mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na
kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Baadhi ya Wasanii kutoka Iran
wakitumbuiza muziki wa Ala wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya
Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam.
Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni
nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na
desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia moja ya vitabu vyenye
maneno ya Kishiraz wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni
baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo
yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya
kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Bibi. Lilian
Beleko, Balozi wa Iran nchini Mossa Farharng na Mkurugenzi wa Kituo cha
Utamaduni cha Iran Ali Bagheri.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akisikiliza maelezo kuhusu michoro ya
Kiutamaduni ya Iran wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni
baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo
yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya
kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
: Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa
Utamaduni wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Benson Mkenda alipotembelea
meza ya Bodi hiyo wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni
baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo
yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya
kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akifurahia jambo mara baada ya kupata
maelezo ya namna ya kufanya marekebisho ya Vitabu kutoka kwa Ali
Navidogooe Shiraz wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni
baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo
yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya
kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akipiga Gitaa lililotengenezwa na
Msaanii wa Uchoraji na Uchongaji Bw. Washington Steven Masanja (kushoto)
wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na
Tanzania jana jijini Dar es Salaam.Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu
ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza
Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”. Kushoto kwa Waziri ni
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Wasanii wa Mashairi Bw. Issa
Amiri Kilimo aka. Kijoka Kidogo na Mwajuma Seleman Yombe wakiimba shairi
kwa njia ya majibizano ikiwa ni kujibu shairi la Siri la mtunzi Haji
Myaka bin Haji la mwaka 1405 jana jijini Dar es Salaam wakati wa kilele
cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran
nchini Tanzania Mossa Farharng akimkabidhi zawadi Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye wakati wa kilele cha Wiki
ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akifurahia jambo na Balozi wa Jamhuri
ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng wakati wa kilele cha
Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng na
baadhi ya viongozi kutoka taasisi za Serikali na ubalozi wa Iran wakati
wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO.
…………………………………………………………
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Serikali chini ya Wizara ya
Hbari Utamaduni Sanaa na Michezo inaendelea na juhudi za kuhakikisha
kuwa Utamaduni wa Mtanzania unakuwa sehemu ya muhimu ya kivutio cha
Utalii ili kutengeneza ajira na kuingizia Serikali mapato.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipokuwa anafungwa
maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi yaliyofanyika jana Jijini
Dar es Salaam ambapo amesema kuwa madhimisho haya yanaimarisha undugu wa
damu wa kiuchumi na kiutamaduni ulioachwa na wahenga.
“Maadhimisho ya wiki ya Utamaduni
wa Shirazi ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwa kwa wairani namna ya
kukuza ,kulinda na kuendeleza Utamaduni,Sanaa,Filamu,Mila na Desturi
zetu”Alisema Waziri Nape.
Aidha ameongeza kuwa Wizara yake
itaweza kufanikisha shughuli za Utamaduni na kuziendeleza kwa
kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya ya nchi kama ilivyofanyika
katika maadhimisho ya mwaka huu kwani yanatangaza vikundi vya Sanaa na
Wasanii.
Kwa upande wa wake Mkuu wa Kituo
cha Utamaduni cha Irani hapa nchini Bw.Ally Baghari amesema kuwa
ushirikiano wa Kiutamaduni baina ya Tanzania na Irani umeongeza
mafanikio ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo hasa kupitia
ubadilishanaji wa Utamaduni tangu enzi za ukoloni.
“Tumejifunza utamaduni wa
kitanzania kupitia maadhimisho haya na tunaamini watanzania pia
wamejifunza utamaduni wa Irani ambao umesaidia kuimarisha ushirikiano
wetu”Alisema Bw Baghari.
Maadhimisho hayo yaliyokuwa na
kauli mbiu “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na
kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
No comments :
Post a Comment