Mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi
Evarist Ndikilo,akionyeshwa ramani ya ujenzi wa mabweni na nyumba za
walimu zinazojengwa katika shule ya sekondari Nasibugani,kulia ni mkuu
wa wilaya ya Mkuranga Gilbert Sanga.
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo,(aliyeinua mkono)
akiangalia ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu zinazojengwa katika shule ya sekondari Nasibugani.
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi
Evarist Ndikilo,akizungumza jambo na wananchi na wanafunzi katika shule
ya sekondari Nasibugani.(Picha na Mwamvua Mwinyi).
………..
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
HALMASHAURI ya wilaya ya Mkuranga
mkoani Pwani,imeokoa kiasi cha sh.bil moja endapo ingetumia wakandarasi
katika ujenzi wa mabweni(5) na nyumba za walimu (5)zinazojengwa shule ya
sekondari ya Nasibugani.
Aidha serikali mkoani
hapo,imelipongeza jeshi la kujenga Taifa (JKT)Ruvu
Mlandizi,Kibaha,kupitia luteni kanal Charles Mbuge,kwa kupelekea vijana
107,wa kujitolea kujenga mabweni na nyumba hizo,kwa gharama nafuu.
Mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,aliyasema
hayo,wakati alipotembelea shule hiyo,kwenda kujionea ujenzi huo
unavyoendelea.
Alisema hadi sasa ujenzi huo umegharimu zaidi ya mil.178 badala ya bil.moja ambazo zingetumika.
Alieleza kwamba ,suala la
kujitolea ni jambo muhimu ndani ya jamii ili hali kujenga ushirikiano
baina ya wananchi,wadau na serikali pasipo kuiachia serikali pekee.
Mhandisi Ndikilo,alisema serikali
inatoa elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne lakini
haimaanishi kuona kuna mambo muhimu ya kuchangia wazazi wakashindwa
kufanya hivyo.
“Sekta ya elimu bado inakabiliwa
na changamoto za miundombinu ikiwemo,upungufu wa nyumba za
walimu,madarasa,maabara,mabweni na matundu ya vyoo”
“Lazima tushirikiane kwa pamoja
tutafute raslimali watu,fedha,kumaliza matatizo haya,tumevulia nguo maji
lazima tuyaoge,hadi kazi hii iishe”alisema mhandisi Ndikilo.
“Na yote haya yanapunguza ufanisi
wa kuinua sekta hii ya elimu,na kutatua kwake vinahitaji fedha nyingi
ambazo halmashauri haziwezi kumudu peke yake”
Mhandisi Ndikilo,alisema endapo
nyumba hizo zikikamilika wataweza kuishi walimu kumi na upande wa
mabweni yatakuwa na uwezo wa kulaza wanafunzi si chini ya 800.
Aliwaomba wadau wa kimaendeleo waendelee kujitokeza kusaidia ujenzi huo ili ukamilike mapema .
Nae mkuu wa wilaya ya Mkuranga,Gilbert Sanga alisema pia waziri wa elimu Profesa Joyce Ndalichako, alitoa kiasi cha sh.mil 250 ambazo zinaendelea kutumika kwenye ujenzi huo.
Alisema mchakato wa ujenzi wa mabweni na nyumba hizo za walimu ulianza baada ya wananchi kuchangia zaidi ya mil.nne .
“Halmashauri ilidai imetenga fedha
kiasi cha sh. mil 32 kwa bweni moja wanafunzi 48 pekee hivyo tuliungana
na kamati ya ulinzi na usalama nao walikubali kuongeza mabweni na mkoa
uliunga mkono”alisema Sanga.
Msimamizi wa ujenzi kutoka kikosi
cha Ruvu JKT,Mohamed Boko alieleza kazi hiyo, ilipangwa kufanyika kwa
miezi miwili lakini imechukua muda .
No comments :
Post a Comment