Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akikata utepe kuashiria Uzinduzi
wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Idara ya Uhamiaji. Mkataba huo ambao
unalenga kuimarisha huduma mbalimbali za Idara hiyo pia umeelekeza
kuanzia sasa Hati za Kusafiria (Pasipoti) zitatolewa kwa siku tano za
kazi kwa watakaoomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja
wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Wapili
kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli.
Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar
es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza na wananchi (wateja)
waliofika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji kabla ya Balozi huyo
hajazindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Idara hiyo. Simba
alisema Mkataba huo unalenga kuimarisha huduma za Uhamiaji ambapo
kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya
mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa
mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Uzinduzi huo
umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (aliyevaa tai) akimsikiliza mteja
aliyefika kupata huduma ya Pasipoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji,
Kurasini jijini Dar es Salaam mara baada ya Balozi huyo kuwauliza
maswali wateja waliofika ofisini hapo. Hata hivyo, wateja hao walisema
wanapewa huduma nzuri na maafisa wa Idara hiyo. Balozi Simba alizindua
Mkataba wa Huduma kwa Mteja ambao unalenga kuimarisha utoaji wa huduma
bora katika Idara hiyo. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara
hiyo, Victoria Lembeli.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza na Watendaji Wakuu wa
Idara ya Uhamiaji nchini kabla ya Balozi huyo kuzindua Mkataba wa Huduma
kwa Mteja ulioandaliwa na Idara hiyo ambao unalenga kuboresha zaidi
huduma zitolewazo na Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana
kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es
Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa
siku zisizozidi kumi. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo,
Kurasini jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto (upande wa pili) ni Kaimu
Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati), akimsikiliza Kaimu
Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli alipokuwa anatoa
maelezo mafupi jinsi Watendaji wa Idara yake walivyouandaa Mkataba wa
Huduma kwa Mteja ambao Balozi huyo aliuzindua Makao Makuu ya Idara hiyo,
Kurasini, jijini Dar es Salaam. Mkataba huo unalenga kuboresha zaidi
huduma zitolewazo na Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana
kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es
Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa
siku zisizozidi kumi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akimkabidhi Vitabu vya
Mkataba wa Huduma kwa Mteja Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara Uhamiaji,
Victoria Lembeli mara baada ya Naibu Katibu Mkuu huyo kuzindua Mkataba
huo katika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es
Salaam leo. Mkataba huyo unaelekeza kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana
kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es
Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa
siku zisizozidi kumi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments :
Post a Comment