Sunday, February 26, 2017

TBL MBEYA INAZALISHA BIA KWA KUTUMIA MAJI MACHACHE KUTOKANA NA TEKNOLOJIA YA KISASA


1 2
Ujumbe kutoka kampuni ya Ishara Consulting wakitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda
4
Moja ya paneli ya kuzalisha umeme wa nishati ya jua katika kiwanda cha Mbeya 
5
Meneja wa Kiwanda cha bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari (aliyeshika simu) akiwaonyesha namna anavyopata taarifa zote muhimu za utendaji kazi wa kiwanda hicho kupitia simu yake ya mkononi ujumbe  kutoka kampuni ya Ishara Consulting Ltd walipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho .
………………………………….
Meneja Mkuu wa kiwanda cha bia cha Mbeya,Jemedari Waziri,amesema kuwa wakati Tanzania inajipanga kuwa nchi ya viwanda kuna umuhimu mkubwa kwa viwanda vilivyo na vipya ambavyo vitajengwa na wawekezaji mbalimbali kuzingatia kanuni bora za uendeshaji wa viwanda lengo kubwa likiwa ni kupunguza athari za uharibifu wa mazingira zinazotokana na mchakato wa uzalishaji katika viwanda.
Jemedari ambaye anaongoza kiwanda hicho ambacho kinashikilia rekodi ya kuwa kiwanda bora cha bia barani Afrika, anasema  TBL Mbeya imefanikiwa kupunguza matumizi makubwa ya maji katika mchakato wa uzalishaji  kutoka hectolita 6  hadi  hectolita 3.2 kwa kila lita moja ya bia inayozalishwa.
Amesema pia kuwa wanafanya uzalishaji kwa kutumia teknolojia za kisasa zinazopunguza uchafuzi wa  hewa (Carbon Emmision) ambao unapelekea kuwepo mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanapelekea kuwepo mabadiliko mbalimbali yanayoleta athari kwa jamii kama vile ukame,upungufu wa maji kutokana na kukauka vyanzo vya maji.
Baadhi ya hatua za kulinda mazingira ambazo kampuni inaendelea kuzitekeleza alizitaja kuwa ni  kutumia teknolojia zisizochafua hewa wakati wa uzalishaji katika viwanda vyake,kushiriki kampeni za kupanda miti na utunzaji wa vyanzo vya maji,kushiriki kampeni za matumizi ya maji kwa umakini kwa kutumia mfumo unaojulikana kitaalamu kama 5Rs,utakatishaji wa maji taka na kuharibu taka ngumu na nyepesi kwa kutumia teknolojia za kisasa ambazo ni rafiki kwa mazingira.
Katika kudhihirisha kuwa tumejipanga kuleta teknolojia za kupunguza athari za uharibu wa mazingira katika uzalishaji katika kiwanda hiki cha Mbeya tayari tumefunga mitambo ya kuzalisha umeme unaotumia nishati ya umeme wa jua na katika kipindi cha muda mfupi mtambo huo umeweza kuzalisha uniti za umeme 15,460 na kupunguza tani za hewa chafu tani 30  na tunategemea kupata mafanikio makubwa zaidi ya kupunguza gharama za matumizi ya umeme na  uchafuzi wa hewa“.Alisema Jemedari.
Kuhusiana na suala la upungufu wa maji unaotishia kuikumba dunia kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa alisema  kampuni inalipa kipaumbele  suala hili na inashirikiana na  serikali, wadau mbalimbali na wananchi kuhakikisha  inaweka mikakati ya  kukabiliana nalo ikizingatiwa kuwa moja ya malighafi kubwa katika uzalishaji wa bidhaa zake ni maji.
Jemedari aliongeza kusema kuwa  kampuni inaliangalia suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji sio kwa kiwango cha  maslahi ya viwanda vyake kupata malighafi  tu bali kwa jamii nzima ambapo kampuni inafanyia biashara  kwa kuwa sera ya kujenga Dunia Maridhawa inashahabiana  Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa  (SDGs)  na suala la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji ni moja ya suala ambalo limepewa umuhimu mkubwa.
Jemedari alimalizia kwa kusema kuwa Tanzania ya Viwanda inawezekana na sekta hii itasaidia kukuza uchumi wa nchi kwa haraka bali kitachotakiwa ni kuhakikisha  viwanda vinatumia mifumo bora ya uendeshaji wa viwanda na kuzingatia matumizi ya teknolojia rafiki  kwa mazingira katika mchakato wa uzalishaji.
Vilevile alitoa wito kwa watanzania wote kuzingatia suala la utunzaji wa mazingira hususani kupanda miti ,kulinda vyanzo vya maji na kutumia maji kwa umakini.

No comments :

Post a Comment