Mkurugenzi wa Barabara, Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Ven Ndyamukama, akitoa hotuba ya
utangulizi katika uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara
zinazotumiwa na magari machache, uliozinduliwa leo jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga,
akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara
zinazotumiwa na magari machache, uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga
(kushoto), akikata utepe kwenye kitabu cha Mwongozo wa ujenzi wa
Barabara zinazotumiwa na magari machache, mara baada ya kuuzindua leo
jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa AFCAP Kanda ya Mashariki na
Kati mwa Afrika, Eng. Nkulule Kaleta.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga
(kushoto), akimkabidhi nakala ya kitabu cha Mwongozo wa Ujenzi wa
Barabara zinazotumiwa na magari machache, mmoja wa wadau waliohudhuria
uzinduzi huo, leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (wa
nne kutoka kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe
waliohudhuria uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa
na magari machache hapa nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
………………..
Serikali imezindua mwongozo wa
mpango na usanifu wa ujenzi wa barabara zinazopitisha magari machache
kwa lengo la kutoa maelekezo na kuwawezesha wahandisi wanaofanya usanifu
wa barabara hizo kutumia gharama nafuu za ujenzi.
Akizungumza katika uzinduzi huo
leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga amesema kuwa
mwongozo huu utakuwa tiba na kuwezesha Serikali kujenga barabara nyingi
na gharama nafuu.
“Ujenzi na ukarabati ya barabara
zinazopitisha magari chini ya 300 kwa siku utakuwa wa gharama nafuu,
kama tutatumia mwongozo huu kwani utasaidia kutatua changamoto
mbalimbali zinazokabili barabara nyingi hususan za vijijini”, amesema
Katibu Mkuu.
Amewataka wahandisi na Mafundi
ujenzi kutumia mwongozo huo katika utekelezaji wa majukumu yao ili
kuweza kusaidia kazi na miradi mbalimbali ya barabara kuweza kufanyika
kwa viwango vilivyo bora na gharama nafuu.
“Hakikisheni wahandisi na Mafundi
ujenzi mnafuata mwongozo huu ipasavyo na kuanzia sasa uwe dira kwenu
katika kazi zenu za kila siku”, amesisitiza Eng. Nyamhanga.
Ameongeza kuwa kutokana na tafiti
mbalimbali zilizofanywa Serikali imegundua uhitaji mkubwa katika mtandao
wa barabara nchini ili kusaidia maendeleo ya kila mwananchi mijini na
vijijini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Barabara katika Wizara hiyo Eng. Ven Ndyamukama amesema kuwa mwongozo
huo unafananua namna ujenzi wa barabara hizo unavyokuwa ikiwemo kujenga
kulingana na idadi ya magari yanayopita.
Ameongeza kuwa Mwongozo huo
unaelekeza kutumia rasilimali chache zilizopo na kuhakikisha masuala ya
mazingira katika maeneo yanayojengwa barabara hizo yatazingatiwa.
No comments :
Post a Comment