Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Steven Kebwe akishiriki katika kazi ya kiwekea mifugo alama ikiwa ni utambuzi wa mifugo hiyo.
Ng’ombe ambao tayari wamesha wekewa alama.
…………………………………………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.
Kebwe Stephen Kebwe amewaagiza Viongozi wa Serikali Mkoani humo ngazi
ya Wilaya hadi kata kuwa na madaftari ya kuwasajiri wakulima ifikapo
Machi 31, mwaka huu.
Dkt. Kebwe ametoa agizo hilo
Februari 22 mwaka huu wakati anatembelea kiwanda cha kuzalisha Mpunga
cha KPL kilichopo katika Wilayani ya Kilombero ikiwa ni sehemu ya ziara
yake ya siku tano aliyoifanya Wilayani humo.
Katika maelezo yake Dkt. Kebwe
amesema zoezi la usajiri wa wafugaji pamoja na mifugo yao lazima liende
sambamba na zoezi la usajiri wa wakulima kwa lengo lilelile la kupata
takwimu halisi kwa Mkoa mzima na si kuwa na takwimu za mezani.
“Sambamba na kazi ambayo
tuliianza mwaka jana mwezi wa sita ya utambuzi wa mifugo kazi ambayo
inaendelea awamu ya pili, madftari ya wafugaji sehemu kubwa yameanza
kuwepo wafugaji wanatambuliwa. Kwa hiyo vitu hivi viwili lazima viende
sambamba hii inasaidia kutengeneza maoteo katika Halmashauri zetu.
Huwezi kufanya maoteo bila kuwa na tax base” alisema Dkt. Kebwe
Mkuu huyo wa Mkoa ameonekana
kuridhishwa na juhudi zinazooneshwa na baadhi ya wakulima hususani wa
Wilaya ya Kilombero kujihusisha katika kilimo na kusema amejionea
mwenyewe watu wamelima mashamba makubwa ingawa mvua zimechelewa kunyesha
tofauti na maeneo mengine ambapo wamelima maeneo madogo.
Hata hivyo amesema ametoa
maelekezo kwa Mkoa wote kufikia tarehe 31 ya mwezi wa tatu kila
Halmashauri iwe na madaftari haya ya wakulima. Hii itatusaidia sana
kujua kiasi mtu anacholima na anachotegemea kuvuna hivyo kuwa na takwimu
zenye uhakika.
Amesema kuwa na madaftari ya
kutunzia takwimu kwa masuala ya kilimo ni maelekezo ya siku nyingi ya
Serikali na ni takwa la kisheria na hiyo inasaidia kupata msingi wa
mapato katika Halmashauri zetu (tax base) kwani bila kuwa na madaftari
hayo takwimu ambazo zitakuwa zinatolewa kwa sehemu kubwa zitakuwa hazina
uhalisia.
Lakini Dkt. Kebwe pia alishauri
uongozi wa kiwanda cha KPL kuwa pamoja na kujishughulisha na kilimo cha
mpunga waongeze jitihada ya kulima zao la mahindi ambalo kwa sasa lina
soko la uhakika na kuwataka pia kuuza ziada ya mahindi watakayoyapata
kwa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula – NFRA.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Kilombero Mhe. James Ihunyo amesema, madaftari ya wakulima na wafugaji
yatasaidia kupunguza kama sio kuondoa kabisa migogoro baina ya wakulima
na wafugaji Kwani Kwa kujua takwimu zao kwa usahihi itasaidia Serikali
kufanya maandalizi ya kutenga maeneo ya kilimo na malisho ya mifugo kwa
usahihi pia, kupitia mradi wa Serikali unaohusika na kupima maeneo yote
ya Ardhi na kuyarasimisha kwa wananchi (Land Tenure supporting Program).
Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kilombero …….Londo amesema, uwepo wa madaftari ya wakulima
kwanza itasaidia kujua idadi ya wakulima wote wa Halmashauri yake,
kujua mazao wanayolima na ukubwa wa mashamba yao pamoja na
takwimunyingine. Lakini pia kuwa na maoteo sahihi ya mazao
yatakayopatikana na tatu kuondoa mchezo mchafu unaofanywa na baadhi ya
wafanya biashara wanaojificha nyuma ya wakulima wakati wa kulipa kodi za
mazao kwani sekta ya Kilimo ndiyo inabeba Halmashauri hiyo kiuchumi.
No comments :
Post a Comment