Dada Neema Mwita Wambura (32)
akizungunza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kupitia njia ya Simu akimshukuru kwa msaada aliompatia wa
kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili. Pia Rais Dkt. Magufuli ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo
pamoja na watoto wake watatu ambao kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia
Rais Dkt. Magufuli alimpatia msaada Dada huyo kiasi cha Shilingi laki
tano. Dada Neema Mwita Wambura aliungua vibaya mara baada ya kumwagiwa
uji wa moto uliokuwa unachemka jikoni na mume wake katika kijiji cha
Kyagata, Tarime mkoani Mara.
Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi
Mwaija ) ambaye amempa hifadhi Neema Mwita Wambura nyumbani kwake
Tandika Davis Corner akiomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu kumshukuru
mara baada ya kuzungumza naye kuhusiana na kumsaidia Dada Neema Mwita
Wambura (32). Rais Dkt. Magufuli amempongeza Mama huyo Mjane ambaye
ameonesha moyo wa kizalendo na kumpa hifadhi Dada huyo aliyemwagiwa uji
wa moto na mumewe katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara. Pia
Rais Dkt. Magufuli alimpa Mjane huyo kiasi cha Shilingi laki tano.
Dada Neema Mwita Wambura (32)
wakwanza kulia akiwa pamoja na Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija )
wakiwa ndani ya gari mara baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli kumsaidaia ili aweze kufanyiwa tena uchunguzi
wa afya yake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
Salaam.
Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili wakimpokea Dada Neema Mwita Wambura (32) na kuanza mara moja
kumfanyia tena uchunguzi wa afya yake katika majeraha aliyoyapata mara
baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa ukichemka jikoni kitendo
kilichofanywa na mume wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru akimjulia hali Dada Neema
Mwita Wambura (32) mara baada ya kufikishwa tena hospitalini hapo. Dada
Neema Mwita alifanyiwa upasuaji mara nne katika siku za nyuma
hospitalini hapo Muhimbili ili kutibu majeraha yake hayo ya moto.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya
dharura na Ajali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma
Mfinanga akizungumza kuhusu hali ya mgonjwa Dada Neema Mwita Wambura
(32) aliyefikishwa tena katika Hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi
wa Afya yake.
Dada Neema Mwita Wambura (32)
akiwa katika hali ya majonzi kufatia majeraha makubwa mwilini mwake
kufatia kumwagiwa uji wa moto na mume wake mkoani Mara.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa
ngozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Ibrahim Mkoma
akizungumzia historia ya mgonjwa huyo ambaye yeye pamoja na jopo la
madaktari bingwa walimfanyia upasuaji ili kutibu majeraha yake ya ngozi
katika kipindi cha nyuma. PICHA NA IKULU
No comments :
Post a Comment